Posts

Showing posts from August, 2024

'CHAPO' KUFANYA UCHAGUZI MDOGO ASUBUHI HII

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ asubuhi hii ya August 31, 2024 wanatarajia kuingia kwenye zoezi la uchaguzi mdogo wa kumchagua Mkurugenzi wao mpya. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Mwanasheria Siti Habib Mohamed, alisema tayari maandalizi yote ikiwemo utoaji wa fomu, maandalizi ya kura yameshakamilika. Alisema, hadi Augost 29 ambayo ilikuwa ndio siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu, kulikuwa na mwanachama mmoja pekee, aliyechukua fomu hiyo. Alisema, tayari dirisha la zoezi hilo, limeshafungwa tokea Augost 29, majira ya saa 8:30 jioni, hivyo tayari kamati yake, imeshaliratibu zoezi hilo, linalitarajiwa kufanyika ofisi ya CHAPO Chake chake asubuhi ya leo. Alieleza kuwa, kwa upande wao, kila kitu kimeshakamilika, na lililobakia kwa sasa ni kuwasubiri wanachama, ambao ndio wapiga kura, kuteleleza wajibu wao. ‘’Kwa upande wa kamati yangu ndo...

TANGAAZO LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FOMU-UCHAGUZI MDOGO CHAPO

Image
  TANGAAZO LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI -CHAPO KAMATI ndogo ya Uchaguzi, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mwanasheria Siti Habib Mohamed, inawatangaazia wanachama wote wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’, kua kuanzia tarehe 26.08.2024,   Tume hiyo imeanza kutoa fomu kwa kila mwanachama wa CHAPO, kwa ajili ya uchaguzi mdogo, wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi wa CHAPO, ambae alifariki Augost 7, mwaka 2024. Fomu hiyo, inapatikana Ofisi ya CHAPO, iliyopo mjini Chake chake, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 jioni kwa siku zote za kazi. Fomu baada ya kujazwa vyema, kama yalivyo maelekezo, itatakiwa kurejeshwa ofisi ya CHAPO, iliyopo Chake chake Pemba, sio zaidi ya tarehe 29.08.2024, saa 8:40 mchana. Ikiwa na vielelezo vifuatavyo: a)     Picha moja ya Mgombea, iliyopigwa hivi karibuni, b)     Ada ya fomu y shilingi 2,500/= ( Shilingi Elfu Mbili Mia Tano tu ) c)  ...

FOMU YA KUOMBA KUGOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI CHAPO

Image
                                                                           FOMU YA KUOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI WA JUMUIA YA WASAIDIZI WA SHERIA CHAKE CHAKE – CHAPO   NB: MALIPO YA FOMU HII NI SHILINGI 2,500/. JINA LA MUOMBAJI: …………………………………………………………………………………                                                                    UMRI ……….. JINSI ………… SHEHIA ……………………………………. JIMBO …………………………….. TAREHE YA KUZALIWA …………/……………./……..………. PAHALA ……………...

WANA 'CHAPO' WAPEWA RAI, KUMKUMBUKA ALIYEKUWA MKURUGENZI WAO

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’, wametakiwa kuendelea kumuombea dua kila wakati, aliyekuwa Mkurugenzi wao Nassor Bilali Ali, na kisha kuiendeleza na kuisimamisha jumuia yao. Wito huo umetolewa leo Augost 17, 2024 na Mratibu Ofisi ya Mufti Pemba, sheikh Said Ahmad Mohamed, kwenye hutuba yake iliyosomwa kwa niaba yake, na sheikh Said Abdallah Nassor, mara baada ya kumalizika kwa dua ya kuombea marehemu huyo, iliyofanyika ukumbi wa Manispaa ya jiji la Chake chake. Alisema, mara baada ya mtu kufariki, yapo mingi yanaweza kumsaidia na moja wapo ni dua za mara kwa mara, kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake. Alieleza kuwa, huu sio wakati kwa wanacha CHAPO, kugawanyika kufuatia kifo cha Mkurugenzi wao, bali waendelee kushikamana, huku wakimkubuka mwenzao kwa dua. Sheikh Said Ahmad Mohamed, alisema kifo cha Mkurugenzi huyo, kamwe kisiwe sababu kwa wao, kufarikiana na kugawanyika makundi mawili, bali ...

'CHAPO' KUSOMA DUA MAALUM

Image
    TAANGAZO LA DUA YA MAREHEMU NASSOR BILALI ALI- ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JUMUIA YA WASAIDIZI WA  SHERIA WILAYA YA CHAKE CHAKE  PEMBA. @@@@ WATU wote na taasisi, wanaalikwa kuhudhuria dua, ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali. Dua hiyo, inatarajiwa kufanyika Ukumbi wa Manispaa ya jiji la Chake chake, ndani ya ukumbi mkubwa. Siku ya Dua hiyo ni Jumamosi ya terehe 17/08/2024 Muda wa kuanza kwa Dua hiyo ni saa 3:00 asubuhi. Kuhudhuria kwako ni muhimu, katika kufanikisha dua hiyo.                       ………..Wabillah Tawfiq…assalaam Alyek….. Tangaazo hili: Limetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uratibu CHAPO – Chake chake Pemba.       +255778921827 Au +255777042182

MAMIA WAMZIKA MKURUGENZI 'CHAPO' SALAMU KILA KONA ZAMIMINIKA

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WASAIDIZI wa sheria wilaya ya Chake chake, wamesema wamepokea salamu za pole kutoka, maeneo kadhaa hapa nchini, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wao, Nassor Bilali Ali, kilichotokea Augost 7, kisiwani Pemba. Akizugumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Jumuiya hiyo Mohamed Hassan, alisema miongoni mwa salamu hizo ni kutoka Afisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utawala Bora Zanzibar. Salamu nyingine, ni kutoka wafanyakazi wa Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria wa Unguja na Pemba, kupitia Mkurugenzi wao Hanifa Ramadhan Said, taasisi za haki za binadamu za Tanzania bara na Zanzibar. Maratibu huyo wa CHAPO alieleza kuwa, salamu nyingine za kuwatakia moyo wa ustahamilivu, zimetolewa na wakurugenzi na wajumbe wa bodi za jumuiya za wasaidizi wa sheria za Unguja na Pemba. Aidha Hassan alisema kuwa, kufuatia kifo hicho, watetezi wa haki za binadamu Pemba, kutoka jumuia za PACSO, TAMWA, ZALHO, Jeshi la Polisi, Mahkama, Mawakili wa kujitegemea na wale...

CHAPO: 'WANANCHI UCHANGANI JENGENI URAFIKI NA WATOTO WENU MTAYAPATA MINGI '

Image
    NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WANANCHI wa kijji cha Uchangani shehia ya Ndagoni wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kujenga urafiki endelevu na watoto wao, ili kugundua kwa haraka, ikiwa wanakumbana na changamoto zikiwemo za udhalilishaji. Ushauri huo umetolewa Augost 6, 2024 na Msaidizi wa sheria wa shehia za Wesha na Ndagoni, Khadija Said Khalfan, wakati akizungumza na wananchi hao, kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria ‘CHAPO’. Alisema, mbinu nzuri kwa wazazi na walezi, ya kugundua mazito wanayopitia watoto wao, wanapokuwa skuli au madrassa, ni kujenga nao urafiki endelevu. Alieleza kuwa, kupitia mpango huo mzazi au mlezi, anaweza kumuuliza maswali kadhaa na majibu yake, yanaweza kumpa mwanga na kujua aina ya marafiki na mwenendo wa mtoto wake kwa ujumla. Alifahamisha kuwa, sio kinga kwa wazazi na walezi, kulalamikia ugumu wa maisha na kuacha kuwatunza watoto na kuwa nao karibu, kwani mazingira yasiorafiki yanazidi kutawala k...

MKURUGENZI CHAPO ATANGULIA MBELE YA HAKI

Image
SOTE NI WA MWENYEZI MUUNGU NA KWAKE TUTAREJEA  Inna lilllahi wainna Ilayih Rajiun........................MKURUGENZI wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, CHAPO Nassor Bilali Ali, amefariki dunia leo Augost 7, 20204 majira ya saa 3:40 akiwa uwanja wa ndege wa Pemba, kwa safari ya kwenda matibabuni hospitali ya Mnazi mmoja. Awali Augost 5, akiwa nyumbani kwake aliumwa na kukimbizwa hospitali ya Vitongoji, ambapo kisha alihamishiwa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani. Augost 7, yaani leo mwaka 2024, alishapata rufaa ya kwenda hospitali ya Mnazi mmoja, ndipo wakati akiwa uwanja wa ndge mauti yalimfikia Maziko yanatarajiwa kufanyika kwao Vikunguni wilaya ya Chake chake majira ya saa 10:00 jioni. Bodi ya wadhamini na wanachama wote wa CHAPO wanamtakia marehemu huyo safari njema na yenye kheir.........