WAGOMBEA CCM JIMBO LA CHAKE CHAKE, KUANZISHA WIKI YA MSAADA WA KISHERIA
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MGOMBEA Ubunge na Uwakilishi jimbo la Chake chake, wamesema kama wakipata ridhaa ya wananchi, wataanzisha wiki ya msaada wa kisheria jimboni humo, ili kuwasaidia wananchi, wenye changamoto za kisheria. Walisema, wanayodhamira ya dhati kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo, wanaondokana na changamoto za kisheria, kwa kuanzisha wiki ya msaada wa kisheria, kila baada ya muda. Wakizungumza na baadhi ya watendaji wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’, wakati walipofika ofisini hapo, walisema wanachosubiri ni ridhaa tu ya wananchi. Wagombea hao walisema, wamebaini kuwa, ipo haja ya kuongeza nguvu ya kutoa elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa wananchi, na hilo litawezekana kwa kuanzisha wiki ya msaada wa kisheria. Mgombea Uwakilishi Abdulla-wahabi Said Abubakar, alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake, na baada ya kukaa na uongozi wa ‘CHAPO’, azma hiyo wanayo. ...