'CHAPO' KUFANYA UCHAGUZI MDOGO ASUBUHI HII
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANACHAMA wa Jumuiya ya wasaidizi wa
sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ asubuhi hii ya August 31, 2024 wanatarajia kuingia
kwenye zoezi la uchaguzi mdogo wa kumchagua Mkurugenzi wao mpya.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi huo Mwanasheria Siti Habib Mohamed, alisema tayari maandalizi
yote ikiwemo utoaji wa fomu, maandalizi ya kura yameshakamilika.
Alisema, hadi Augost 29 ambayo ilikuwa ndio siku ya
mwisho ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu, kulikuwa na mwanachama mmoja pekee,
aliyechukua fomu hiyo.
Alisema, tayari dirisha la zoezi hilo, limeshafungwa
tokea Augost 29, majira ya saa 8:30 jioni, hivyo tayari kamati yake, imeshaliratibu zoezi hilo, linalitarajiwa kufanyika ofisi ya CHAPO Chake chake asubuhi ya leo.
Alieleza kuwa, kwa upande wao, kila kitu
kimeshakamilika, na lililobakia kwa sasa ni kuwasubiri wanachama, ambao ndio wapiga
kura, kuteleleza wajibu wao.
‘’Kwa upande wa kamati yangu ndogo ya uchaguzi, tuko sawa na
hakuna jambo ambalo hatujalifanya, kazi iliyobakia ni kwa wapiga kura kutumia haki yao,’’alieleza.
Mjumbe wa kamati hiyo ya uchaguzi Hafidh Abdi Said, alisema zoezi la uchukuaji wa fomu, ambalo lilianza Augost 26, 2024 limekwenda vyema, na hukukua na changamoto yoyote.
Uchaguzi huo mdogo, unafuatia kifo cha marehemu
Nassor Bilali Ali, ambae alikuwa Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria
wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ aliyefariki Augost 7, mwaka huu, wakati
akiwa uwanja wa ndege, kwa safari ya kwenda matibabuni Unguja, baada ya kuugua
ghafla.
Kisha marehemu, alizikwa kijijini kwao, Vikunguni
wilaya ya Chake chake siku hiyo hiyo, majira ya saa 11:15 jioni, Mwenyezi Muungu….
ailaze roho ya marehemu pahala pema, peponi aminaaa…
Mwisho
Comments
Post a Comment