Posts

Showing posts from June, 2024

KILELE WIKI YA MSAADA WA KISHERIA: MAKAMU WA PILI AAGIZA JUMUIYA ZA WASAIDIZI WA SHERIA ZIPATIWE OFISI

Image
  NA HAJI NASSOR, UNGUJA@@@@ MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdull, amesema nia yake ni kuona jumuiya zote za wasaidizi wa sheria, zinakuwa na ofisi ambazo hazitolipa kodi, kwani msingi wa kazi zao, ni wa kujitolea. Makamu huyo wa Pili, aliyasema hayo leo Juni 28, 2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria, kilichofanyika ukumbi wa Idrisaa Abdull-wakil mjini Unguja. Alisema, kama hatua zimeshachukuliwa kwa jumuiya za wasaidizi wa sheria wilaya ya Kusini na Kaskazini ‘A’ kuwa ofisi na jumuiya nyingine tisa zilizobaki, lazima hilo lifanyike. Alieleza kuwa, kwa vile msingi mkuu wa wasaidizi wa sheria ni wa kujitolea, hakuna budi kwa serikali, kuhakikisha inajitolea na kuwapatia ofisi, ili wafanye kazi zao kwa ufanisi. ‘’Nitawatuma wasaidizi wangu, kukutana na uongozi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, ili kukaa pamoja na kuona kila wilaya, imetoa jengo kwa ajili ya ofisi za wasaidizi wa sheria,’’alieleza. Katika h...