Posts

Showing posts from June, 2023

‘’MLIOPEWA MAFUNZO WA SHERIA WAWI WAHAMASISHENI WANANCHI KUDAI HAKI ZAO’' CHAPO

Image
  NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@ KAIMU Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, ‘CHAPO’ Kassim Ali Omar, amewataka wahitimu wa mafunzo ya sheria, kutoka shehia ya Wawi, kuwahamasisha watu kudai haki zao mbali mbali. Wito huo aliutoa leo Juni 19, 2023 Vikutani shehiani humo, kwenye ufungaji wa mafunzo ya siku ya tano, ya sheria kwa wajumbe wa kamati ya sheha na kamati nyengine, za shehia ya Wawi. Alisema, anaamini kwa mafunzo hayo, washiriki hao watakuwa waalimu wazuri kwa wenzao, katika kuwahamasisha kudai haki zao mbali mbali badala ya kuwakatisha tamaa. Alieleza kuwa, ndani ya mafunzo hayo wamejua mambo ambayo yanaweza kusababisha kesi kufutwa, kuondolewa au mtuhumiwa kutumikia kutiwa hatiani. ‘’Mimi naamini kwa mafunzo haya mliopewa ya sheria ngazi ya shehia, mtakuwa na uwezo kuwahamasisha wale waliokata tamaa, kwenda kudai haki zao, mbali mbali,’’alieleza. Katika hatua nyingine, Kaimu Mwenyekiti huyo wa Bodi ya wadha...

WAWI WAUKUBALI USHAURI WA MSAIDZI WA SHERIA UJENZI WA OFISI YA SHEHA

Image
  NA MWANDISHI WETU, CHAPO@@@@ UONGOZI wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, umesema umeridhia usahuri wa Msaidizi wa sheria wa Jimbo la Wawi, la kutaka kuanzisha ujenzi wa ofisi ya sheha, shehiani humo. Ulisema, wazo la Msaidizi wa sheria wamelipokea mikono miwili, kwani imekuwa ni usumbufu wanapokuwa na mikutano yao mbali mbali, hasa katika kipindi cha jua au mvua. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, leo Juni 16, 2023 Sheha wa shehia hiyo Sharifa Waziri Abdalla, alisema baada ya kulifikisha wazo hilo kwa wajumbe wake, wamelipokea na kusema linawezekana mno kutekelezwa. Alisema, fikra hiyo imekuja wakati mwafaka, wakati serikali kuu nayo ikihimiza ujenzi wa ofisi za masheha, ili sasa waondokane na kufanyakazi kwenye makaazi yao. Alieleza kuwa, wazo hilo ambalo aliahidi kulisimamia, linaweza kutekelezwa, hasa kwa umoja na mshikamano, uliopo ndani ya shehia ya Wawi. ‘’Ni kweli tumeupokea na kuukubali ushauri wa Msaidizi wetu wa sheria wa Jimbo la Wawi, la kuomb...