ZIARA YA ‘CHAPO’ YAFUFUA BARAZA LA WATOTO CHANJAANI
NA MWANDISHI MAALUM, PEMBA@@@@ UONGOZI wa shehia ya Chanjaani wilaya ya Chake chake Pemba, umesema ujio wa wasaidizi wa sheria kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilayani humo, umewasaidia kutambua dhana ya baraza la watoto kisheria, kinyume na hapo awali. Hayo yameelezwa juzi na Sheha wa Chanjaani Khatib Ali Vuai, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, baada ya kumalizika kwa kikao, kilichojumuisha wasaidizi wa sheria, wajumbe wa sheha na askari shehia na kufanyika Chanjaani Gereji. Alisema, hapo awali hakuwa na uwelewa mpana, wa nini maana ya baraza la watoto, utataratibu wake, aina ya wajumbe, idadi, kazi zao, utambuzi wake kisheria, ingawa ujio wa wasaidizi wa sheria umemfungua macho. Alieleza kuwa, alikuwa anasikia tu ndani ya shehia yake, kuwa kuna baraza la watoto, ingawa alidhani ni suala lisilotambuliwa kisheria, na hakuwa na hamu ya kulifuatilia kwa undani. Alifahamisha kuwa, kikao hicho cha wasaidizi wa s...