Posts

Showing posts from May, 2023

‘CHAPO’ YAWAKOSHA WANANCHI KILINDI ELIMU YA SHERIA

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa kijiji cha Kuungeni shehia ya Kilindi wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema mfumo uliofanywa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ kuwafuata kijijini kwao na kuwapa elimu ya kisheria, inafaa kuendelezwa. Walisema, mfumo huo unafaa kuendelezwa na kuwa imara zaidi, kwani umewasaidia katika kukuza uwelewa wao, hasa masuala la haki na fursa zao kisheria. Wakizungumza kwenye mkutano wa wazi, uliofanyika Mei 14, 2023 kijijini hapo, walisema wamepata uwelewa wa mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na maana ya wizi kisheria. Wananchi hao walisema, wamejua njia ambazo mwananchi anaweza kuingia kwenye kosa la wizi, ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vya wizi, kuficha taarifa pamoja na kumpa mawasiliano. Mwananchi Massoud Juma Khamis, alisema ujio huo wa watendaji wa CHAPO, umewaamsha katika ufahamu pia wa masuala ya udhalilishaji, ule ambao sio maarufu kwa jamii. Alieleza kuwa, kutopeleka huduma za kibinadamu ambazo...

WASAIDIZI WA SHERIA 'CHAPO' WAKUMBUSHWA JAMBO MUHIMU

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WASAIDIZI wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, wakumbushwa kuwahudumia wananchi kwa kuwapa elimu, ushauri na msaada wa sheria, ili iwe rahisi kupata ufumbuzi wa haki zao. Ushauri huo umetolewa leo Mei 7, 2023 na Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, wakati akizungumza na wasaidizi hao wa sheria, kwenye kikao maalum cha mwezi, kilichofanyika ofisini kwao. Alisema, lazima wasaidizi hao wa sheria waelewa kuwa, wajibu wao kwa jamii, ni kuendelea kuwahudumia kila siku na kila wakati, kwani wamekuwa wakiwategemea katika kuapata haki zao. Alieleza kuwa, ndio maana CHAPO kwa kushirikiana jumuiya nyingine, imekuwa ikiwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wasaidizi hao wa sheria, ili wawe na uweledi wanapokutana na jamii. Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa, wapo wananchi ambao wameshakata tamaa ya kupata haki zao, hivyo ni wajibu wa wasaidizi wa sheria, kuwapa ushauri ili kutimiza ndoto zao. ...