‘CHAPO’ YATIMIZA AHADI KWA WANAMICHEZO WAWI
NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ WANAMICHEZO shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, wametakiwa kujiepusha na matumizi ya vilevi kama vile dawa za kulevya, kwani kufanya hivyo, wanaweza kuzima ndoto zao mapema kwenye michezo. Ushauri huo umetolewa na Msaidizi wa sheria wa shehia hiyo Fatma Hilali Salim, Septemba 9, 2025 shehiani humo, wakati akizungumza na wanamichezo hao na wananchi wingine, kwenye hafla ya kukabidhi mipira, iliyotolewa na Mkurugenzi Idara ya Katiba na Msaada wa sheria pamoja na Katib Mtendji wa Baraza la Vijana Zanzibar. Alisema, moja ya njia nyepesi kwa mwanamichezo yeyote ili asifikie ndoto zake kwenye michezo, ni matumizi ya dawa za kulevya, ambazo ni hatari kwa afya yake. Alieleza kuwa, dawa za kulevya sio tu kwamba zinazima ndoto kimichezo, lakini zinamshushia heshima, kutoonekana binaadamu kamili, kutoaminika katika jamii yake. ‘’Dawa za kulevya kwa mwanamichezo ni sumu ya kutokusonga mbele, maana hao munaosiki ni wachezaji wakubwa, walianza kuwa ...