MVUMONI CHAKE CHAKE WAOMBA KUONANA NA DK. MWINYI
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Mvumoni wilaya ya Chake chake, wameomba kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ili kumfikishia kilio chao cha ya kucheleweshewa fidia zao, katika utanuzi wa uwanja wa ndege Pemba. Walisema, walifanyia tathmini za nyumba, miti na vipando vyengine tokea mwaka 2015, juu ya utanuzi wa uwanja wa ndege Pemba, ingawa hadi leo, hawana taarifa rasmini juu ya tathmini hiyo ilipofikia. Wakizungumza mbele ya watendaji wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ waliofika shehiani hapo, kutoa elimu na msaada wa kisheria, walisema sasa uvumilivu umewashinda. Wananchi hao walisema, kwa sasa hakuna kiongozi ambae anaweza kuwapa maelekezo na wakayakubali, isipokuwa awe ni Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi pekee. Walisema kiongozi huyo amekuwa mkweli na mtendaji kwa vitendo, hivyo wameziomba mamlaka husika, kuzungumza nae ili awasili shehiani humo, na kumpa ...