CHAPO: WANANCHI CHAKE CHAKE ENDELEENI KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA
NA HAJI NASSOR, PEMBA JUMUIYA ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chakechake 'CHAPO' imewakumbusha wananchi wilayani humo, kuendelea kushirikiana na makarani wa sensa, ili kufanikisha zoezi hilo. Wito huo umetolewa leo August 25, mwaka 2022 na Mkurugenzi wa 'CHAPO' Nassor Bilali Ali wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu kuelekea zoezi linaloendelea la sensa ya watu na makaazi. Alisema ni vyema kwa wananchi kuhakikisha wanaandaa na kupanga shughuli zao vizuri, ili makarani wa sensa watakopfika kutaka taarifa iwe rahisi kupatikana. Mkurugenzi huyo alisema zoezi hilo huja kila baada ya miaka 10, hivyo ni wajibu kwa wananchi kufurahia na kushiriki vyema, ili serikali iweke mipango na mikakati yake vyema vya maendeleo. "Wananchi wa wilaya ya Chakechake tunawaomba kuwa tayari zoezi hilo la sensa limeshaanza tokea August 23, mwaka huu, hivyo ni wajibu kwao kushirikiana na masensa pale watakapofika kwenye maeneo yao kwa kuhesabiwa,"alisema. Katika hatua ...