Posts

Showing posts from January, 2023

MDHAMINI KATIBA, SHERIA: 'AWAPA TANO WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA'

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: AFISA Mdhamini wizara ya nchi afisi ya rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali, amesema kazi inayofanywa na wasaidizi wa sheria na watoa msaada wa kisheria, imesaidia kuonesha jamii njia ya haki na kuacha batili. Afisa Mdhamini huyo aliyaeleza hayo, ukumbi wa wizara hiyo, kwenye mkutano wa robo mwaka, wa masuala ya msaada wa kisheria, ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar. Alisema, licha ya changamoto kadhaa walizonazo watoa na wasaidizi hao wa msaada wa kisheria hao, lakini kwa sasa hali inaridhisha ya wananchi, kuzijua haki zao mbali mbali. Alieleza kuwa, jamii awali haikuwa na uwelewa mpana wa haki zao mbali mbali, lakini baada ya Idara ya Katiba na Msaada wa sheria kuwajengea uwezo na kisha kwenda mtaani, hali inaridhisha. ‘’Kwa haki bado msingi mkuu kwa jamii kuzipata na kuzijua haki zao zitabakia kuwa, zimeimarisha na watoa na wasaidizi wa sheria waliomo shehiani, kwa hili hongere ni,’...

CHAPO: 'WANAFUNZI WAIBUWENI WANAOTAKA KUWADHALILISHA'

Image
  NA MWANDISHI MAALUM, CHAPO WANAFUNZI wa chuo cha Qur-an cha kijiji cha Vikutani shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kuwaibua ndugu na jamaa zao, wanaoashiria kutaka kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji. Ushauri huo umetolewa Januari 29, 2023 na Msaidizi wa sheria Jimbo la Wawi Haji Nassor, wakati akitoa elimu ya kupambana na matukio ya ukatili na udhalilishaji, hasa kwa watu wao wa karibu, kwenye mkutano uliofanyika chuoni hapo. Alisema, tafiti kadhaa zinaonesha kuwa, sasa watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo na watu wao wa karibu, na kushindwa kutoa taarifa hizo, katika maeneo husika. Alieleza kuwa, wakati umefika sasa kutowafumbia macho watu hao, kwani wamekuwa wakishindwa kuonesha upendo wa kweli kwao, jambo ambalo linaweza kusababisha kupoteza mwelekeo wa maisha yao. ‘’Wanafunzi niwasihi sana kuwa, iwapo kuna kaka, baba, ami, mjombo ameanza kukufanyia vitendo vya udhalilishaji, mseme kwa wenzako au wetu wengine wa karibu,’’alifafanua. Aidha...

MSAIDIZI MPYA WA SHERIA JIMBO LA WAWI AKARIBISHWA

Image
  NA AMINA AMHED, PEMBA:: UONGOZI wa  Shehia ya Wawi Jimbo la Wawi wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba,  umesema utatoa kila aina ya ushirikiano  na msaidizi wao mpya wa sheria, katika kutatua changamoto mbali mbali za jamii zikiwemo matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikikosa ufumbuzi, kwa kutokuwepo msaidizi wa sheria.  Hayo yalielezwa Januari 22, 2023 na Sheha wa Shehia ya Wawi Sharifa Ramadhan Abdalla, alipokuwa akifungua mkutano maalum wa kutoa Elimu  kwa wajumbe wa sheha wa shehia hiyo, kutoka kwa Msaidizi moya wa sheria Kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Chake Chake Pemba 'CHAPO'.     Alisema anaamini kuwa Idara ya Katiba na Masaada wa Kisheria kumuwezesha Msaidizi huyo wa sheria, haikukosea, kwani amemuwa mtendaji mzuri na mfuatuliaji hata kabal ya kupata mafuanzo ya awali ya sheria na sasa kuijiunga na CHAPO  na kuwa katika shehi hayo.   Alisema kwa...

IDARA KATIBA NA MSAADA WA KISHERIA YAUKARIBISHA MWAKA 2023

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: WANANCHI kisiwani Pemba, wametakiwa kuufanya mwaka mpya wa 2023, uwe wa mageuzi kwa kupunguza matukio ya ukatili na udhalilishaji, kwa kuwatumia wasaidizi wa sheria, ili kupata elimu, ushauri na msaada wa kisheria.   Kauli hiyo imetolewa Januari 7, 2023 na Afisa sheria, kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar, ofisi ya Pemba Bakari Omar Ali, wakati akizungumza na mwandishi hizi, katika kuukaribisha mwaka mpya.   Alisema, matukio ya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto bado yalikuwa yameshika kasi kwa mwaka 2022, hivyo amewataka wananchi, kwa huu 2023 uwe mwaka wa mageuzi kwa kupunguza matukio hayo.   Alieleza kuwa, Idara inaowasaidizi wa sheria katika kila jimbo, la uchaguzi, hivyo ni vyema wakawatumia ili kupata uwelewa wa kisheria, sambamba na elimu ya kupambana na matukio hayo.   Afisa sheria huyo alifafanua kuwa, wasadizi hao wa sheria, wako tayari na saa yoyote kutoa elimu na msaada wa kis...

CHAPO: WASAIDIZI WAPYA WA SHERIA MASHEHA NDIO WENYEJI WENU SHEHIANI

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: WASAIDIZI wapya wa sheria wa majimbo ya wilaya ya Chake chake kisiwani Pemba, wametakiwa kushirikiana na masheha kwenye shehia zao, ikiwa wanata kufanikiwa katika kazi zao, za utoaji elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa leo Januari 27, 2023 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Safia Saleh Sultan, wakati akizungumza na wasaidizi hao, ofisini hapo mjini Chake chake. Alisema, kila msaidizi wa sheria, mwenzake katika shehia yoyote ile ni Sheha wa shehia husika, kwani ndie mwenyeji wake kikazi, na si vyema kumdharau. Alieleza kuwa, kazi ya msaidizi wa sheria moja ya wajibu wake, ni kuhakikisha anafanyakazi bega kwa bega na sheha au wajumbe wa sheha, ili kufanikisha kazi zao zake. ‘’Mnakwenda kwenye shehia, lakini muelewe kuwa, msishahu kuwa Sheha ndio mwenyeji wako, na usijaribu kufanya jambo lolote, pasi na kumuomba ruhusa,’’alieleza. Katika hatua...

WANAFUNZI WA MADRASSA CHAKE CHAKE WAONESHWA NJIA KUJIKINGA NA UDHALILISHAJI

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: IDARA ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, ofisi ya Pemba, imewakumbusha wanafunzi wa madrassa za qur-an kisiwani Pemba, kujitenga mbali na watu wanaowanesha dalili za vitendo vya udhalilishaji, ikiwa ni pamoja na kuwawekea picha chafu kupitia simu zao. Kauli hiyo imetolewa leo Januari, 7 2023 kwa nyakati tofauti, na mwakilishi wa Idara hiyo Mohamed Massoud Said, wakati akizungumza na wanafunzi wa madarassa za Vikunguni na Machomane wilaya ya Chake chake, kwenye ziara maalum, ya kutoa elimu ya kupambana na matendo hayo.  Alisema, moja ya dalili ya mtu anaetaka kumdhalilisha mtoto huanza kwa kumuonesha picha za ngono, kumnunulia zawadi, kumpa fedha, na kuendelea kwa maneno ya ushawishi juu ya udhalilishaji. Alisema ni jukumu lao, kwanza kutoshirikiana na watu wa aina hiyo, hata ikiwa ni wazazi wao, au kutoa taarifa kwa watu wengine, kabla ya kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji. Mwakilishi huyo wa Idara ya Katiba na msaada wa kisheria, aliwataka w...