CHAPO YAWAONESHA NJIA WANA WAWI KUEPUKA MIGOGORO YA ARDHI
NA ASHA ABDALLA, PEMBA WANANCHI wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake, wametakiwa kutafuta hatimiliki kutoka serekalini, maratu baada ya kununua kiwanja, shamba au kipande cha aina yoyote cha ardhi, ili kuepukana na migogoro isiyokuwa ya lazima. Hayo yameelezwa Oktoba 28, 2023 na Mjumbe wa Bodi kutoka Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, ‘CHAPO’ Asha Sleiman Said, wakati akizungumza na wananchi hao, kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na jumuiya hiyo na kufanyika Kunguni Wawi. Alisema kua, zipo njia mbali mbali zinazotumiwa ili mtu aweze kupata haki ya kutumia ardhi bila ya migogoro yoyote, ikiwemo njia yakununua na kupewa hati ya matumizi. Alieleza kuwa, migogoro mingi ya ardhi husababishwa na watu kukosa hati za matumizi pamoja na kuwekeana mipaka inayoondoka kama vile miti na mifimbi ya mito na maziwa. Mjumbe huyo kutoma CHAPO, alifahamisha kuwa, mwarubaini pekee mara baada ya mtu k...