Posts

Showing posts from December, 2023

BARAZA LA WATOTO WESHA, LAWATUNISHIA MISULI WASHUGHULIKIAJI KESI ZA UDHALILISHAJI

Image
    NA MWANDISHI MAALUM, CHAPO@@@@ BARAZA la watoto wa shehia ya Wesha wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema vitendo vya ukatili na udhalilishaji vitaendelea kuwepo na kuwaathiri, kwa vile watendaji, washughulikiaji, watoaji hukumu, wapelelezi na madaktari ni watu wazima na sio katika kundi lao. Walisema, wapo watoto wenzao wamedhalilishwa na wengine kupata ulemavu wa kudumu na hata kusababisha vifo, ingawa kesi hizo, zinapopelelezwa na kufikishwa mahakamani, watuhumiwa huachiwa huru. Hayo wameyasema Disemba 17, 2023 kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ na kufanyika uwanja wa mikutano nyumbani kwa sheha wa shehia ya Wesha, wilayani humo. Wamesema, inashangaaza kuona kesi zinazowahusu watoto kudhalilishwa au kufanyiwa ukatili, zinapelelezwa na kutolewa ushahidi, ingawa kisha hufutwa na kuwaacha wao na maumivu. Katibu wa Baraza hilo Zainab Kassim Juma, alisema kwa vile watoto ndio wanaodhalilishwa na ...

USHAURI WA KISHERIA WA 'CHAPO' WAZAA MAKAAZI YA KUDUMU KWA MJANE

Image
  HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ZAKIA Rashid Baraka (36) wa Chanjamjawiri wilaya ya Chake chake, anaetgemewa na watoto sita, sasa amejengewa makaazi ya kudumu na aliyekuwa muume wake, baada ya kunufaika na ushauri wa kisheria, aliyopewa na wasaidizi wa sheri wilaya ya Chake chake. Mjane huyo, alisema baada ya kuachika na aliyekuwa muume wake na kisha kumtaka ahame ndani ya nyumba waliokuwa wamejenga pamoja kijiji cha Tundaua shehia ya Kilindi wilayani humo, alimua kufuatilia haki yake kwa wasaidizi wa sheria. Alisema, kisha mwanamme huyo alikutanishwa nae, na kutakiwa kunijenga chumba kimoja, kwa vile alishakataa kumpa chumba kimoja katika nyumba walipokuwa pamoja kindoa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, nyumbani kwake Chanjamjawiri, alisema katika ujenzi wa nyumba hiyo anayoishi muume wake kwa sasa alitumia nguvu kazi na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 1. Alisema kuwa, alitegemea sana baada ya kuchwa aidha engerejeshewa fedha ama kupewa haki yake ya chumba kimoja, ingawa ...

CHAPO: NA MIAKA SABA YA MAPAMBANO YA UKATILI, UDHALILISAJI CHAKE CHAKE

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ CHAPO, ni kifupi cha Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba. Ukiwa mtaalamu wa lugha sema ‘Chake chake Paralega Organization’ kwa ufupi ni CHAPO. CHAPO, sio neno geni masikioni mwa wakaazi wa wilaya ya Chake chake, wanaoishi ndani ya shehia 32, ikiwemo za Vitongoji, Wesha na Chanjaani, inayobebwa na majimbo ya Chake chake, Ole, Ziwani, Chonga na Wawi. Kwamba, humu ndio eneo la CHAPO inapofanyakazi, tena kupitia wanachama wake, ambao ni wasiaidizi wa sheria tena waliosajiliwa na kutambuliwa. Kwa sasa, si haba kuanzia mwaka 2018, serikali imeshapitisha sheria rasmi, iliyokuja kuweka mambo yawe ‘ shega’ mazuri ya wasaidizi wa sheria. Maana, ipo sheria maarufu ya Msaada wa Kisheria Zanzibar nambari 13 ya mwaka 2018, ambayo awali ilitanguliwa na sera ya mwaka 2017, ambayio imekuja kumueleza nani Msadizi wa sheria? Kwamb, ni yeyote aliyepata mafunzo ya awali ya sheria, na kisha kusajiliwa, na Idara ya Katiba na Msaada wa Ki...