MSAIDIZI WA SHERIA WAWI, AKAGUZWA ARDHI INAYODAIWA KUVAMIWA NA SERIKALI
NA MWANDISHI WETU, CHAPO@@@@ MKURUGENZI wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Nassor Bilali Ali, amewataka wamiliki wa ardhi wanaoishi mbali nazo, kujenga utamaduni wa kuzikagua kila, wakati, ili kuepushwa kuvamiwa . Mkurugenzi huyo aliyasema hayo Machi 24, 2023, eneo Kwasharifuali shehia ya Wawi, wakati akizungumza na walalamikaji wa eneo hilo, walilodai kuvamiwa na Kiwanda cha mafuta ya makonyo zaidi ya miaka sita sasa, kwa shughuli za upandaji wa miti ya biashara. Alisema, ardhi iliyokaa bila ya kuendelezwa na kisha mmiliki kushindwa kuipitia kila wakati, huwa rahisi mtu yeyote kuanzisha matumizi. Alieleza kuwa, kama mmiliki anaishi mbali na ardhi husika, ni vyema wakaanzisha uwakala wa ulinzi wa ardhi zao, ili iwe rahisi kupatikana taarifa kwa aina yoyote ile ya matumizi. Mkurugenzi huyo wa CHAPO alisema, wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu kwa wananchi mbali mbali, juu ya umuhimu wa matumizi ya ardhi. ‘’Wananachi tunawashauri kama wana ardhi ambaz...