CHAPO: ‘WAZAZI CHAKE CHAKE MSIWARUHUSU WATOTO KUOMBA 'MKONO WA IDD’
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JUMUIYA ya wasaidizi wa sheria, wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’, imewataka wazazi na walezi wilayani humo, kuwakataza watoto, kuacha utamaduni wa kuomba fedha za sikukuu ‘ mkono wa idd’ katika maeneo ya mbali na wanapoishi. Kauli hiyo imetolewa leo Mei 26, 2026 na Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo jana, Mohamed Hassan Abdalla, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, kuelekea sherehe ya sikukuu ya kiislamu. Alisema, utamaduni wazazi kuwaruhusu watoto wao kuomba fedha kipindi cha sikukuu, huwa ni chanzo kikuu cha udhalilishaji ambao unaepukika. Alieleza kuwa CHAPO, inawapenda mno watoto wa wilaya hiyo, na ndio maana, inaendelea kuwasisitiza wazazi na walezi wao, kuondokana na mpango huo. Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, kwani wapo baadhi ya vijana na hata watu wazima, wanaweza kuchukua fursa hiyo ya kuwadhalilisha watoto hao. ‘’Wapo baadhi ya watoto wanatoka kijiji kimoja hadi chingine, kisa ni siku ya sikukuu, hugonga kila nyumba kuomba fedha ‘ mkon...