MKURUGENZI CHAPO ATANGULIA MBELE YA HAKI
Inna lilllahi wainna Ilayih Rajiun........................MKURUGENZI wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, CHAPO Nassor Bilali Ali, amefariki dunia leo Augost 7, 20204 majira ya saa 3:40 akiwa uwanja wa ndege wa Pemba, kwa safari ya kwenda matibabuni hospitali ya Mnazi mmoja.
Awali Augost 5, akiwa nyumbani kwake aliumwa na kukimbizwa hospitali ya Vitongoji, ambapo kisha alihamishiwa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani.
Augost 7, yaani leo mwaka 2024, alishapata rufaa ya kwenda hospitali ya Mnazi mmoja, ndipo wakati akiwa uwanja wa ndge mauti yalimfikia
Maziko yanatarajiwa kufanyika kwao Vikunguni wilaya ya Chake chake majira ya saa 10:00 jioni.
Bodi ya wadhamini na wanachama wote wa CHAPO wanamtakia marehemu huyo safari njema na yenye kheir.........


Comments
Post a Comment