Posts

Showing posts from December, 2022

MKURUGENZI 'CHAPO' AONA MBALI KWA WASAIDIZI WA SHERIA

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA MKURUGENZI wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, amesema wakati umefika sasa, kwa sheria ya Msaada wa kisheria Zanzibar, kuweka kipengele cha kuwaruhusu wasaidizi wa sheria, kuingia mahakamani kuwawakilisha wateja wao.   Alisema, kwa elimu yao inafaa sana sheria iwaruhusu kuingia mahakama za mwanzo na wilaya, ili wanapokuwa na kesi za mwananchi, na ikifikia wakati wa kwenda mahakamani, sheria iwaruhusu.   Mkurugenzi huyo aliyasema hayo Disemba 19, 2022, kwenye mkutano kwa njia ya zoom wa kuwasilisha utafiti wa awali, wa haki ya mwanamke kumiliki mali, uliofanywa Tanzania bara na Zanzibar, kupitia tasisi ya LSF.   Alisema, wakati mwengine wasaidizi wa sheria wamekuwa wakiianza na kuendeleza vyema kesi husika, lakini hukorogeka na mwananchi kukosa haki yake, kwa kule kushindwa kujieleza mahakamani.   Alieleza kuwa, wakati mwengine sio kila lalamiko mfano la ardhi, huduma, ...

MSAIDIZI WA SHERIA WESHA AWAPA MBINU WANAWAKE MALEZI YA WATOTO

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: WANAWAKE wa kijiji cha Kaole, shehia ya Wesha wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kujitathimini aina ya malezi wanayowarithisha watoto wao, ikiwa ni mwafaka, kwa ajili ya kuyamudu mazingira yao, ya kupambana na majanga mbali mbali, kama ya ukatili na udhalilishaji.   Ushauri huo umetolewa Novemba 5, mwaka 2022 na Msaidizi wa sheria wa shehia za Wesha na Ndagoni wilayani humo, Khadija Said Khalfan wakati akizungumza na wananchi hao, kwenye mkutano wa wazi wa kutoa elimu, ndani ya siku 16 za kupinga ukatili, mkutano ulioandaliwa na Jamuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’.   Alisema, kila utafiti unaofanywa, umekuwa ukiwaangukia wanawake, kuwa wamelengaza kamba katika malezi, na wapo baadhi yao, wamekuwa wakiwarithisha malezi mabovu watoto wao.   Alieleza kuwa, kwa mfano wapo wanawake wamekuwa wakiwafichia uovu hasa watoto wa kike, na kujenga uadui kwa baba yao, jambo ambalo halimsaidii mtoto, katika mais...

KONGAMANO SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI, WATOTO MIAKA 14 HADI 17 PASUA KICHWA

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: MAHAKAMA maalum ya kupamba na makosa ya ukatili na udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, imesema kesi za udhalilishaji zinazowahusu watoto wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 17, ndio pekee zinazowatesa wao na ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka, kwa kule kukataa kutoa ushahidi. Kauli hiyo, imetolewa Novemba 2, mwaka 2022 na Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, wakati akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuali yalioulizwa na wananchi, kwenye kongamano la kuelekea siku 16 za kupinga ukatili, lililofanyika Kiwanda cha Makonyo Wawi. Alisema, mara matukio hayo yanapotekezea kwenye jamii, wazazi wao huwa na ari, kasi na hamu ya kuyafikisha mbele ya vyombo vya sheria, ingawa baada ya muda, hawaonekani mahakamani. Alisema, na hasa kesi za aina hiyo zinazowaweka njia panda ni zile zinazowakabili watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 17, ambao kimatendo ni watu wazima. ‘’Hao wanaobahatika kufika mahakamani, basi wakati wa kutoa ushahidi hueleza kuwa, wale wa...