WASAIDIZI WA SHERIA, WAWI ZIWANI WACHANJA MBUGA
NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ JITIHADA za pamoja na endelevu zinahitajika, ili kuwajenga watoto katika mazingira ya malezi bora katika jamii, kwa lengo la kujinasua na majanga yanayowazunguruka. Hayo yameelezwa hivi karibuni na Msaidizi wa Sheria kutoka shehiya ya Wawi Haji Nassor Mohamed, alipokuwa akiwasilisha mada juu ya haki za watoto na wajibu wao, kwa wanafunzi wa A lmadrassatul- Muuminina Syyidat Aishaa , iliyopo Fletini shehia ya Wara wilaya ya Chake chake. Alisema kila mmoja ana haki zake na wajibu wake katika maisha ya kila siku hivyo kukiwa na malezi ya pamoja, jamii itakuwa na mazingira bora ya kuishi kwa watoto wa leo na kesho. ”Haki zenu watoto moja wapo ni kupatiwa elimu kama hii ya Madrassa,skuli, pia kupewa majina mazuri, kupatiwa huduma nyengine mbali mbali ambazo haziharibu taratibu za mila na desturi,"alisema. Katika hatua nyingine, Msaidizi huyo wa sheria shehia ya Wawi, Haji Nassor Mohamed, aliwataka wanafunzi hao kufua...