CHAPO: 'WAZAZI ONGEZENI ULINZI KWA WATOTO KIPINDI HICHI CHA MAPUMZIKO'
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKURUGENZI wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Mohamed Hassan Abdalla, amewataka wazazi na walezi, kuwa makini na kufuatilia nyenendo za watoto wao, kwa kukinga na majanga kama ya uudhalilishaji, hasa kipindi hiki cha mapunziko ya masomo. Alisema, wahalifu waliowengi wamekuwa wakijisogeza na maeneo ya watoto wanamopenda kucheza cheza, hivyo ni vyema kwa wazazi na walezi wakaimarisha ulinzi mara dufu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Novemba 15, 2024, Mkurugenzi huyo, alisema wakati huu wa skuli zikiendelea na mitihani ya taifa, kundi kubwa la watoto wapo majumbani, hivyo ni vyema ulinzi ukaimarishwa. Alieleza kuwa, wadhalilishaji wanaweza kujichanganya na watoto wakiwa kwenye michezo mbali mbali, hivyo ni wajibu ulinzi dhidi yao, ukaongezwa. ‘’Nitowe wito na tahadhari kwa wazazi na walezi, katika kipindi hiki wakiwa watoto hawaendi masomoni, na kutawanyika mtaani hovyo hovyo, ni kuongeza ulinzi, ili ...