SHEHIA YA MVUMONI WAZINDUA KAMATI YA KUPINGA UDHALILISHAJI
NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ MKUU wa Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii Pemba, Omar Mohamed Ali amesema kuwa kuundwa kwa kamati ya kupinga na kupambana na vitendo vya udhalilishaji, itasaidia kwa kiasi kikubwa, kuandaa jamii yenye ustawi bora ambayo itawaweka wanawake na watoto, katika mazingira yaliyosalama. Alisema kuwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, bado vinaendelela kujitokeza katika jami, hivyo serikali, inaendelea kutumia mbinu tofauti, ikiwemo kuunda kamati za shehia, wilaya, mkoa na taifa, ili kupambana na na vitendo hivyo. Aliyasema hayo katika uzinduzi wa kamati ya kupinga udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto shehia ya Mvumoni, hafla iliyofanyika skuli ya sekondari ya Furaha. Alieleza kuwa, kuwepo kwa vitendo hivyo vimekuwa vikiwarudisha nyuma, baadhi ya jamii kwa kuona muhali wa kuviripoti, hivyo uwepo wa kamati hiyo inaweza kuwa mwarubaini. "Nendeni mkafanye kazi kwa kuielimisha jamii, juu ya athari ya vitendo vya ukatili ...