MRAJISI WA NGOs: ‘ZAPONET’ JIPANGENI KUJITEGEMEA WENYEWE
NA HAJI NASSOR, UNGUJA@@@@ MRAJISI wa asasi za kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla, amesema mtandao wa wasaidizi wa sheria Zanzibar ‘ZAPONET’ ianze sasa kujipanga vyema kuhakikisha wanajiendesha wenyewe, na sio kutegemea wafadhili. Mrajisi huyo aliyasema hayo leo Januari 25, 2026 ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe Unguja, wakati akiufungua mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka ‘ZAPONET’, uliokuwa na malengo kadhaa, ikiwemo mapatio ya katiba na uwasilishaji wa ripoti za wanachama wao. Alisema, ZAPONET ni muhimili muhimu kwa jumuia za wasaidizi wa sheria, lakini kikubwa kwa sasa ni kujipanga mapema, ili kujiendesha yenyewe na kutoa usaidizi kwa wanachama wao. Alieleza kuwa, msingi wa wasaidizi wa sheria kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria kwa jamii bila ya malipo, inazingalia sana jumuia zao pamoja na mtandao huo, katika kuwajengea uwezo. Alifafanua kuwa, ingawa kwa sasa wanaendelea kushikwa mkono na taasisi ya LSF, na kufanya vizuri katika utendaji wao wa kazi. ‘’...