WANACHAPO WAPEWA MAFUNZO AKILI MNEMBA 'AI'
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya akili ya kisayansi ‘akili mnemba’, baada ya watendaji wa wawili wa jumuiya hiyo, kumaliza mafunzo kama hayo, wiki iliyopita. Kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa ‘CHAPO’ Mohamed Hassan Abdalla, alisema utaratibu kwa sasa utakuwa kwa kila atakayerudi kwenye mafunzo, kuhakikisha anawapa na wenzake. Alisema, mpango huo ulikuwepo zamani, ingawa katika siku za hivi karibuni, ulionekana kufa, na wakati umefika sasa kuufufua, ili kuona nguvu zinazotumiwa na washirika wao, zinaungwa mkono. Akitoa mada ya mafunzo hayo ofisini kwao Chake chake jan August 17, 2025, alisema akili mnemba, ni mfumo wa kompyuta ambao umeshajazwa taarifa kadhaa, ambazo ni za ukweli, kwa ajili ya matumizi. Alisema, utaalaamu baada ya kuendelea, mifumo hiyo hujazwa taarifa rasmi, na kisha kwa kutumia mifumo ya tovuti za ‘GPT’, unaweza kuipakua na kuuliza mas...