WANAKONGAMANO: ‘RUSHWA MUHALI ITAENDELEA KUTUTAFUTA MAPAMBANO DHIDI YA UDHALILISHAJI’
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAATHIRIKA wa matendo ya ukatili na udhalilishaji kisiwani Pemba, wamesema pamoja na juhudi za serikali kuweka mazingira ya kupungua matendo hayo ikiwemo kuweka adhabu kali, bado rushwa muhali ni kikwazo katika jamii. Wakizungumza kwenye kongamano la siku moja la kuelekea siku 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji, lililoandaliwa na Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba CHAPO, na kufanyika ofisi ya TAMWA Chake chake, washiriki hao walisema bado rushwa muhali ni changamoto. Walisema bado katika jamii, suala la rushwa muhali linaendelea kujitokeza, hali inayosababisha kuimarika kwa matendo ya ukatili na udhalilishaji. Hidaya Mjaka Ali kutoka Umoja wa watu wenye Ulemavu UWZ, alisema, serikali imezirekebisha sheria, kwa kuongeza adhabu ya kuanzia miaka 30 na kuendelea. Alieleza kuwa kama hilo lipo, ni wajibu sasa kwa mahakim na majaji kuzifuata sheria hizo, wakati wa kutoa hukumu, waathirika wapate imani na vyombo vya s...