Posts

Showing posts from September, 2023

CHAPO: ‘WARIPOTINI WAZAZI, WAALIMU, WAJOMBA WANAOTAKA KUWADHALILISHA''

Image
  NA MWANDISHI WETU, PEMBA WANAFUNZI wa chuo cha Kur-an cha Kichangani shehia ya Mgogoni Jimbo la Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba, wamekumbushwa kuwaripoti wazazi, waalimu, walezi na watu wengine, wanapoona dalili za wao, kutaka kudhalilishwa . Walieleza kuwa, moja ya dalili hiyo ni mtu huyo kuongeza mapenzi ya kupindukia, kumpa zawadi zisizotarajiwa na kumshika shika sehemu nyeti za mwili wake, ikiwemo kifuani na makalio. Ushauri huo umetolewa na Msaidizi wa sheria, Jimbo la Wawi Fatma Hilali, wakati akizungumza na wanafunzi hao na waalimu, kwenye mkutano wa wazi, wa utoaji elimu, juu ya namna ya kujikinga na majanga yakiwemo ya udhalilishaji. Aliwaambia wanafunzi hao kuwa, dalili nyingine ni kupigwa mabusu sehemu tofauti za mwili, kupewa fedha na hasa na mtu asiyemjua pamoja na kupakatwa. ‘’Wanafunzi mkiona kuna dalili za kawaida, mtu anakushika kwenye mashavu, makalio, kifuani, mbavuni, anakupa pesa na hasa kwa mtu wa nje, pipi toweni taarifa kwa waalim au wazazi,’...

WASAIDIZI WA SHERIA 'CHAPO' WATOA UJUMBE KWA WANAFUNZI

Image
  Na, Hassan Msellem, Pemba   WANAFUNZI skuli ya Sekondari ya Dk. Salim Ahmed Salim iliyopo Wara wilaya ya Chake -chake Pemba, wametakiwa kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji na utumiaji wa dawa kulevya, ili kufikia malengo waliojiwekea.   Akitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wanafunzi hao   Septemba 11, 2023, Msaidizi wa Sheria shehia ya Wawi Haji Nassor Mohamed, alisema tafiti zinaonesha kuwa, waathirika wakuu wa vitendo hivyo, ikiwemo ubakaji, ulawiti na ukatili wa kijinsia, ni wanafunzi skuli.   Aidha amewasihi wanafunzi hao, kuwatumia wasaidizi wa Sheria, ili kupata ufumbuzi juu ya changamoto mbali mbali za kisheria, zinazowakabili.   "Udhalilishaji ni kumfanyia mtu kitendo chochote, ambacho kitamuathiri kimwili, kiakili au kisaikolojia, hivyo ni vyema mkajiepusha na hili,’’alieleza.   Nae Msaidizi wa Sheria Jimbo la Wawi Fatma Hilal, amesema miongoni mwa sababu zinazochangia baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na maso...