WATOTO WASAKATA SOKA WESHA WALALAMIKIA KUTENGWA MATUMIZI YA UWANJA
NA MARYAM NASSOR, PEMBA@@@@ BARAZA la watoto wa shehia ya Wesha wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema changamoto yao ya kukatazwa matumizi ya uwanja wa mpira wa miguu nyakati za jioni, inawanyima fursa ya kujiendeleza, kimichenzo. Walisema kuwa, changamoto hiyo inawarudisha nyuma kimichezo, kwani hawapati muda mzuri katika kufanya mazoezi yao. Hayo, yameelezwa na mjumbe wa kamati hiyo, Saidi Mohamed Ali, kwenye mkutano wa wazi, uliyoandaliwa na Jumuiya ya wasaidizi wa Sheria wilaya ya Chake chake (CHAPO), uliofanyika huko Wesha kwa Sheha. Alisema, watoto katika kijiji chao, wana malengo makubwa katika soka, kutokana na kuwa, mpira siku hizi ni ajira na biashara pia. Alisema kuwa, vijana wengi siku hizi wamefanikiwa kujipitia ajira kupitia soka, hivyo nao kuendelea kubanwa na timu kubwa wasifanye mazoezi, kwenye uwaja pekee uliopo Wesha, ni kuanza kuzizima ndoto zao. ‘’Kila mmoja asubuhi anakwenda kwenye harakati, sasa jioni ndio wakati ...