Posts

Showing posts from July, 2024

CHAPO: 'WAPENI ELIMU YA KINGA WAZAZI WIZI WA WATOTO'

Image
    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ JUMUIYA ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ imewakumbusha wasaidizi wa sheria wilayani humo, kutilia maanani, elimu kwa jamii, juu ya wimbi la wizi wa watoto lililoibuka hivi karibuni. Kauli hiyo imetolewa leo Julai 27, 2024 na Afisa Ufuatiliani na Tathmini kutoka ‘CHAPO’ Wahida Kombo Khamis, kwenye kikao cha mwezi cha kuwasilisha ripoti za elimu na msaada wa kisheria, kilichofanyika ofisini kwao mjini Chake chake. Alisema, pamoja na kuwaelimisha wananchi juu ya udhalilishaji, migogoro ya ardhi, ndoa, wizi, dawa za kulevya pamoja na kuhubiri amani, lakini watilie mkazo, juu ya elimu ya tahadhari ya wizi wa watoto. Alieleza kuwa, ijapokuwa kwa wilaya ya Chake chake halijakua la kutisha jambo hilo, kama ilivyo kwa baadhi ya mikoa ya Tanzania bara, lakini ni vyema, kinga ikaanza kuwekwa. Alifahamisha kuwa, hilo ni miongoni mwa majukumu ya wasaidizi wa sheria, hivyo ni wakati sasa kulieleza kwa upana, ili jamii ifahamu...

‘WANAWAKE MSIONGOZE VIKAO VYA SULHU KESI ZA UDHALILISHAJI’

Image
  NA ALI KHAMIS, PEMBA@@@@ MJUMBE wa sheha wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, Mwanajuma Bakar Mohamed, amewataka wanawake wa kijiji cha Mchekeweni, wasikubali kuongoza vikao vya sulhu, inapotokeza changamoto ya udhalilishaji wa watoto. Alisema, imebainika wapo baadhi ya wanawake wamekuwa ndio watandikaji majamvi na mikeka, ili kuandaa mchakato wa sulhu, kwenye kesi za udhalilishaji. Mjumbe huyo, aliyasema hayo jana kwenye madrassa ya wanawake iliyopo kijijini hapo, wakati wa mkutano wa wazi, ulioandaliwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’, ikiwa ni mkutano wa kawaida wa utoaji wa elimu. Alieleza kuwa, ni vyema sasa wakakimbilia vituo vya kisheria, ili kutoa taarifa haraka, mara tu inapotokeza changamoto ya ukatili na udhalilishaji. ‘Sisi akinamama, ni kweli tumeumbwa na huruma kubwa, lakini sio katika eneo hilo, na wala tusijihusishe na sulhu, kwani kufanya hivyo, ni kumuuza mtoto wako kwa thamani ndogo,''alieleza. Katika hatua n...

BONANZA: WATOTO YARIPOTINI MAJANGA MNAYOFANYIWA

Image
  NA HASINA KHAMIS, OUT- PEMBA@@@@ MKURUGENZI Mtendaji wa Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba ‘TUJIPE’ Tatu Abdalla Msellem, amesema watoto wana haki ya kulindwa na kulijinda wenyewe, kutokana na majanga mbali mbali, yakiwemo ya udhalilishaji kwa kuyaripoti kwa wazazi na Serikali pale awapofanyiwa vitendo hivyo .   Alisema, kulingana na mazingira ya sasa baadhi ya wazazi wamekuwa mbali na watoto wao, na ndio chanzo cha udhalilishaji na ukatili wanaofanyiwa watoto hao.   Aliyasema hayo jana Julai 21, 2024 katika bonanza la Mabaranza ya watoto lililofanyika skuli ya Istikama Mkanjuni wilaya ya Chake Chake, lilioandaliwa kwa ushirikiano na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’.   Aidha aliwataka kujilinda, kusimamia na kujitetea katika suala la udhalilishaji na mazingira yao wanayoishi, ili kuepukana na vitendo hivyo.   "Kumekuwa na mtindo wa watoto kudhalilishana, hivyo ninawaomba kuacha mara moja kufanya vitendo hi...

CHAPO: 'WATUMIENI WASAIDIZI WA SHERIA WALIOMO SHEHIANI MWENU'

Image
  MARYAM SALUM, PEMBA@@@@. WANANCHI wa shehia ya Mgogoni wilaya ya Chake Chake, wametakiwa kuvitumia vyombo vya sheria vilivyomo ndani ya shehia zao, wakiwemo wasaidizi wa sheria, ili kueleza changamoto zinazowakabili za kisheria kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi. Kauli hiyo ilitolewa jana Julai 14, 2024 na Msaidizi wa sheria wa shehia hiyo Fatma Hilali Salim, wakati akizungumza na wananchi hao katika skuli ya maandalizi Ditia shehiani humo, ikiwa ni muendelezo ya mikutano ya wazi inayoendeshwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake Chake Pemba 'CHAPO'.  Alisema kuwa sasa hivi jamii, imekuwa ikikabiliwa na matatizo mengi yakiwemo ya udhalilishaji pamoja na migogoro ya ardhi, jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa jamii.  Alieleza kuwa, kutokana na changamoto hizo na nyengine kama hizo, kuna haja jamii kutumia vyombo vya sheria vilivyomo kwenye shehia zao, akiwemo sheha na wasaidizi wa sheria kueleza kero zao, ili kupatiwa ufumbuzi wa kisheria na si  kwa n...

MJANE AIPA TANO ‘CHAPO’ KUMPA MTAJI

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MJANE wa watoto watatu mkaazi wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake, ameishukuru Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilayani humo ‘CHAPO, kumuwezesha kwa mtaji wa shilingi 70,000 na kuanza biashara. Alisema hakutarajia kua, ombi lake la shilingi 70,000 kwa uongozi wa ‘CHAPO’ lingejibiwa kwa haraka, ambalo alitamani kuanzisha biashara ya uji na mandazi, akiamini ndio itakayomsadia kimaisha. Mama huyo aliyasema hayo, jana wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kufuatia kutekelezewa ombi lake kwa CHAPO alilolitoa Juni 25, mwaka huu kwenye shamra shamra ya wiki ya msaada wa kisheria. Alisema, tokea akabidhiwe mtaji wa shilingi 70,000 Juni 27, sasa anaendelea vizuri na kujipatia faida, kati ya shilingi 3,500 hadi shilingi 4,000 kwa biashara ya uji na mandazi kwa siku. ‘’Kwa hali yangu ya kipato, mimi nikipata shilingi 4,000 huwa shilingi 2,000 nazihifadhi na hadi sasa nimeshatimiza shilingi 32,000 kama faida, sio jambo dogo kwangu,’’alifa...

JUMUIYA ZA WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA: 'WIKI YA MSAADA YA KISHERIA ILICHAPUZA KAZI ZETU'

Image
    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAKURUGENZI wa Jumuiya za wasaidizi wa sheria kisiwani Pemba, wamesema wiki ya msaada wa kisheria iliyomalizika mwezi uliopita kisiwani Unguja, ilichapuza utendaji wao wa kazi, kwa jamii. Wakizungumza kwenye kikao cha tathmini kilichofanyika leo Julai 5, 2024 ukumbi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Chake chake, walisema waliongeza hamasa ya kutoa elimu kwa jamii. Walieleza kuwa, ijapokuwa hilo ni jukumu lao la msingi, lakini kuanzia Juni 25 hadi 27, mwaka huu, waliwafikia wananchi wengi zaidi, kuliko ilivyozoeleka. Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria Micheweni ‘MIDIPAO’ Saleh Hamad alisema kwa kushirikiana na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria, walilifikia kundi la walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini, Micheweni. Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Mkoani ‘MDIPAO’ Nassor Hakim Haji, alisema walipanga kuwafikia wandesha boda boda 65, ingawa walivuuka lengo hilo. ‘’Kwa mfano, sisi tulitaraji...