TANGAAZO LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FOMU-UCHAGUZI MDOGO CHAPO
TANGAAZO LA UCHUKUAJI
NA UREJESHAJI FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI -CHAPO
KAMATI
ndogo ya Uchaguzi, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mwanasheria Siti Habib
Mohamed, inawatangaazia wanachama wote wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya
ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’, kua kuanzia tarehe 26.08.2024, Tume hiyo imeanza kutoa fomu kwa kila
mwanachama wa CHAPO, kwa ajili ya uchaguzi mdogo, wa kujaza nafasi ya
Mkurugenzi wa CHAPO, ambae alifariki Augost 7, mwaka 2024.
Fomu hiyo,
inapatikana Ofisi ya CHAPO, iliyopo mjini Chake chake, kuanzia saa 3:00 asubuhi
hadi saa 9:00 jioni kwa siku zote za kazi.
Fomu baada
ya kujazwa vyema, kama yalivyo maelekezo, itatakiwa kurejeshwa ofisi ya CHAPO, iliyopo
Chake chake Pemba, sio zaidi ya tarehe 29.08.2024, saa 8:40 mchana.
Ikiwa
na vielelezo vifuatavyo:
a) Picha moja ya Mgombea, iliyopigwa
hivi karibuni,
b) Ada ya fomu y shilingi 2,500/= (Shilingi
Elfu Mbili Mia Tano tu)
c) Nambari ya usajili ya uanachama.
d) Saini ya Mdhamini wako.
PIA
fomu hiyo inapatikana kupitia.
FOMU YA KUOMBA KUGOMBEA NAFASI YA MKURUGENZI CHAPO
(chapo24.blogspot.com)
NB: ANGALIZO KWA WAGOMBEA
-Fomu itakayojazwa
kwa kalamu isiyokuwa BULUU, AU kujazwa kwa herufi NDOGO, kukozeshea maadishi au
isiyokuwa na ADA haitozingatiwa na Tume.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Mwenyekiti wa Tume +255777679747
au Katib +255778921827

Comments
Post a Comment