Posts

Showing posts from December, 2025

WAJUMBE SHEHIA MVUMONI WAPIGWA MSASA ELIMU YA KISHERIA

Image
    NA MWANDISHI WETU, PEMBA   WAJUMBE wa sheha wa shehia ya Mvumoni wilaya ya Chake chake, wameelezwa kuwa, suala la haki za binaadamu sio la kuomba, bali ni haki ya kila mmoja, kwa ubinaadamu wake.   Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilayani humo ‘CHAPO’ Mohamed Hassan Abdall, aliyasema hayo leo Disemba 7, 2025 wakati akiwasilisha mada ya haki za binaadamu, kwa wajumbe hao, kwenye mafunzo ya siku moja.   Alisema, haki za binaadamu, ni haki zote anazostahiki mtu, kwa sababu ya kuwepo kwake duniani, ikiwemo uhai, matibabu, afya, elimu, utaifa na uzalendo.   ‘’Niwaombe sana wajumbe wetu wa shehia ya Mvumoni, kwanza elimu hii mkawafikishie na wingine, maana haki za binaadamu ni zote,’’alieleza.   Akizungumzia faida za kufanya sulhu kwa kesi za madai kama vile, huduma za mke, watoto, migogoro ya ardhi, mirathi na madeni, alisema inaondosha visasi. Alifahamisha, kuwa ndio maana, wamempeleka msaidizi wa sheria katika eneo lao...

SHEHIA YA MVUMONI YAPATA MSAIDIZI MPYA WA SHERIA

Image
  NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ MSAIDIZI mpya wa sheria shehia ya Mvumoni wilaya ya Chake chake Pemba, Haji Nassor Mohamed, ameuomba uongozi wa shehia hiyo, kumpa kila aina ya uhirikiano, ili kufanikisha majukumu yake.   Ameyasema hayo Novemba 29, 2025 alipokuwa akijitambulisha kwa wajumbe wa sheha, mara baada ya kuhamishiwa shehia hiyo akitokea Wawi, kwa lengo la kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria bila ya malipo.   Alisema kuwa, kubwa analohitaji ni ushirikiano kuanzia kwa sheha, wajumbe na wananchi wa Mvumoni, ili lengo la kuwahudumia wananchi lifikiwe.   Alieleza kua, ataendelea kuwa tegemeo kwa wananchi wa Mvumoni, kwani anaamini wapo ambao hawana uwelewa mpana, wa masuala ya kisheria.   ‘’Kwanza nishukuru kwa kupokelewa, na ninachotaka kubwa zaidi ni umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwenu,’’alieleza.   Aidha Msaidizi huyo wa sheria, aliwakumbusha wajumbe hao wa sheha, kutokubali kuzifanyia sulhu kesi za jinai na hasa z...