Posts

Showing posts from November, 2025

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA @@@@ AFISA Mdhamini wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Pemba, Halima Ali Khamis, ameitaka Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar ‘AGCZ’ kurudi tena kwa wadau, baada ya kuyachakata maoani ya sheria nambari 13 ya mwaka 2018 ya Msaada wa Kisheria Zanzibar.   Mdhamini huyo aliyasema hayo leo Novemba 13, 2025 , ukumbi wa wizara ya Fedha Pemba, alipokuwa akifungua kikao kazi, cha kukusanya maoni ya sheria ya Msaada wa Kisheria, mbele ya wadau wakiwemo wasaidizi wa sheria, Polisi, Masheha na wadau wa haki za binaadamu. Alisema itapendeza zaidi, baada ya kukusanya maoni hayo kwa Afisi ya Mwanasheria Mkuu kurudi tena kwa wadau, ili kujadiliana kabla ya kuandikwa, kama sheria ya msaada wa kisheria. Alieleza kuwa, wadau wanataka kuona maoni yao, ikiwa yamezingatiwa kwa kiasi gani, kwenye uandikwaji wa sheria hiyo upya hapo baadae. ‘’Niwaombe sana wenzetu wa ofisi ya 'AGCZ', mkumbuke kurudi tena kwa wadau, baada ya kukusanya ...