Posts

Showing posts from November, 2022

MKURUGENZI 'CHAPO' AWAVUTIA PUMZI WAJUMBE WATORO WA VIKAO

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: MKURUGENZI wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, ameelezea kusikitishwa kwake na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, kukumbwa na dharura kila panapoitishwa vikao.   Alisema, wapo baadhi ya watendaji sasa wamekuwa ndio ugonjwa wao usio na tiba wa kutohudhuria vikao, jambo ambalo kwa baadhi ya wakati, hurejesha nyuma mipango na mikakati yao.   Mkurugenzi huyo ameyasema hayo, Novemba 5, mwaka 2022,  ofisini kwake mjini Chake chake, wakati akizungumza na watendaji wake, kwenye kikao cha robo ya nne ya mwaka.   Alisema vikao ni sehemu muhimu ya kutengeneza, kuunda au kuamua jambo husika kwa maslahi ya wananchi wa wilaya ya Chake chake, sasa ikiwa kuna wajumbe ni wagonjwa kwa dharura wanaweza kukwamisha jitahada.   Alisema kuanzia sasa ‘CHAPO’ itakuwa wakali kwa wajumbe watoro na wasiopenda kufuata wakati wa vikao husika, kwani kinyume chake, wanaweza kukwamisha baadh...

LSF: YATOA MAAGIZO MAZITO KWA CHAPO

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA MFUKO huru wa msaada wa kisheria ‘LSF’ umeutaka uongozi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ kufanyakazi zao kwa umakini mkubwa, ili kuendeleza sifa yao ya utendaji kazi.   Ushauri huo umetolewa Novemba 1, mwaka 2022 na Afisa Program Mwandamizi kutoka mfuko huo Zanzibar, Alphonce Marandu Gura, wakati akizungumza na watendaji wa ‘CHAPO’ ofisini kwao mjini Chake chake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kujitambulisha kwa jumuia za wasaidizi wa sheria kisiwani Pemba.   Alisema, anayotaarifa ya uchapaji kazi wa watendaji wa CHAPO, hivyo amewakumbusha kuendelea kufanyakazi kwa uweledi na ushirikiano, ili waendelee kujijengezea saifa kwao na jamii kwa ujumla.   Alisema, CHAPO ni tegemeo kubwa la wananchi wa wilaya ya Chake chake, hivyo lazima waelewa thamani hiyo, na kuithamini katika kazi zao za kila siku.   Alieleza kuwa, kazi ya kuihudumia jamii ni nzito na inakuwa na changamoto kadhaa, na wa...