'WALINDENI WATOTO NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA'
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa kijiji cha Birikau shehia ya Michungwani wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kuwalinda watoto wao, kwani watumiaji, wasafirishaji na waingizaji wa dawa za kulevya, wamekuwa wakiwatumia watoto, katika kufanikisha malengo yao. Ushauri huo umetolewa April 30, 2024 na Askari kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Chake chake, anayezifanyia kazi shehia za Wesha, Michungwani na Ndagoni wilayani humo Khamis Ali Khamis, wakati akizungumza na wananchi, kwenye mkutano wa wazi. Alisema, kwa sasa watumiaji na wasafirishaji wamekuwa wakiwatumia watoto, wakijua kuwa, kisheria hawashatakiwa na wakati mwingine hawawezi kupekuliwa. Alieleza kuwa, taarifa zipo zinazoenesha kuwa, sasa watoto wamekuwa wakitumiwa na watumiaji, wasaambazaji wa dawa za kulevya, baada ya mitego ya kuwatumia watu wazima kugundulika. ‘’Wazazi wa kijiji ch Birikau, kuweni makini mno na wasambaazaji, watumiaji, wauzaji na waingizaji wa dawa za kulevya, sasa wamehamishia kazi hiy...