Posts

Showing posts from July, 2025

WANANCHI 422,908 WAFIKIWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA

Image
  NA HAJI NASSOR, UNGUJA@@@@ WANANCHI 422,908 wakiwemo wanawake 209,185 na wanaume 213,723 wamefikiwa na elimu na msaada wa kisheria, kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, iliyomalizika hivi karibuni Zanzibar. Kampeni hiyo, iliendeshwa katika mikoa yote mitano ya Zanzibar, inayojumuisha wilaya 11, ambapo miongoni mwao kati ya waliofikiwa, ni wanawake, watu wenye ulemavu, vijana, wazee na wanafunzi. Hayo yalielezwa leo Julai 16, 2025 na Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Zanzubar, Mwinyi Talib Haji, kwenye hutuba yake, iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Mwanasheria mkuu Shaaban Ramadhan Abdalla, kwenye kilele cha maadhimisho ya jukwaa la tano, kilichofanyika Michenzani Mall. Alisema, kwa takwimu hiyo na kazi iliyofanywa, inadhahirisha umoja na mshikamano, unaosababishwa na uwepo wa Muungano wa Tangayika na Zanzibar. Alieleza kuwa, serikali inafurahishwa mno kuona wananchi walio wengi na wanyonge, wanaendelea kupata msaada, ushauri na elimu ya kisheria bila ya ...

WANAFUNZI JIFUNZENI KUSEMA ‘NO’ MSIDHALILISHWE

Image
    NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wa skuli ya msingi na sekondari ya kiislamu ya Amini, iliyopo Wesha wilaya ya Chake chake, wametakiwa kujifunza kusema hapana, wanapoona kuna ishara za wao kutaka kudhalilishwa. Ushauri huo, umetolewa leo Julai 14, 2025 na Askari shehia Khamis Ali Khamis, wakati akizungumza na wanafunzi hao, kwenye shamra shamra za wiki na jukwaa la msaada wa kisheria, mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya wa saidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’ na kufanyika skulini hapo. Alisema, wasiwe rahisi mno wanapoona kuna viashiria vya udhalilishaji, hivyo wajifunze kwa vitendo neno la kukataa, ili kujikinga na madhara makuwa zaidi. ‘’Niwaombe leo mkutano huu wa wazi ulioandaliwa na wenzetu CHAPO, na tukiwa ndani ya wiki na jukwaa la msaada wa kisheria, ninawaomba mjifundishe kusema hapana, mkihisi mazingira hayako salama,’’alisema. Aidha, aliwataka wanafunzi hao, kuchukua muda mkubwa wa kujisomea, kuliko jambo jingine lolote. Nae Msaidizi...