CHAPO YAPOKEA WASAIDIZI WA SHERIA WAPYA, YAWAPA NENO
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JUMUIYA ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba CHAPO, imewapokea wasaidizi wa sheria wapya na kuwahakikishia ushirikiano wa hali ya juu, ili kufikia malengo ya kuihudumia jamii, wilayani humo. Hayo yalielezwa leo Machi 30, 2024 na Mkurugenzi wa ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, wakati wa ukaribisho na mapokezi ya wasaidizi wapya watatu wa sheria, kutoka shehia za Michungwani, Kibokoni na Mgelema, hafla iliyofanyika ofisi ya CHAPO, mjini Chake chake. Alisema, C HAPO inafarajika mno kuona sasa inaongeza idadi ya wasaidizi wa sheria 21, kutoka 18 wa awali, jambo ambalo linaendelea kupunguza ukakasi kwa shehia 11, zitakazobakia bila ya kuwa na wasaidizi wa sheria, kati ya zote 32 za wilaya hiyo. Alieleza kuwa, wasaidizi hao wa sheria wapya, watapewa kila aina ya ushirikiano, wakati huu wa miezi mitatu wakiwa kwenye majaribio na hata baada ya kumaliza na kuanza kazi rasmi shehiani mwao. Mkurugenzi Nassor alifafanua kuwa, wananchi wa vijiji wana...