Posts

Showing posts from February, 2023

MWAKILISHI WAWI ABARIKI CHAPO KUANZISHA DARASA LA SHERIA KWA WANANCHI

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Bakar Hamad Bakar, ameunga mkono, wazo la wasaidizi wa sheria Jimbo la Wawi, la kutaka kuanzishwa darasa maalum la kutoa elimu ya sheria, kwa wananchi wa shehia ya Wawi jimboni humo. Alisema, wazo la wasaidizi hao wa sheria, kutaka kuanzisha darasa maalum, ni jambo la msingi, kwani elimu waliyopatiwa wao, itasambaa kwa upana. Mwakilishi huyo aliyasema hayo, Febuari 19, 2023 wakati akizungumza na uongozi wa shehia ya Wawi, kwenye kikao maalum cha maandalizi ya darasa hilo. Alisema, wananchi wanahitaji kupata elimu ya kujua haki na wajibu wao kwa jamii, samba mba na kupata uwelewa wa mambo ya kisheria. ‘’Kwanza niunge mkono wazo ambalo wenzetu hawa wasaidizi wa sheria Jimbo la Wawi, wameliwaza na mimi nitaunga mkono kwa hali na mali, ili kufanikisha darasa hilo,’’alieleza. Katika hatua nyingine, Mwakilishi huyo wa Jimbo la Wawi aliwataka wasaidizi hao wa sheria, kuhakikisha darasa hilo linakuwa endelevu, kwa kundi jing...

WASAIDIZI WA SHERIA WAWI: 'VIJANA MSICHEZE CHEZE NA WATOTO OVYO OVYO WATAWAUMBUA'

Image
  NA MWANDISHI MAALUM, CHAPO MSAIDIZI wa sheria Jimbo la Wawi Haji Nassor Mohamed, amewatahadharisha vijana wa shehia ya Wawi, kuacha kucheza cheza na watoto, kwani huwa rahisi kuwataja mara wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji. Kauli hiyo ameitoa Febuari 19, 2023 uwanja wa mpira wa miguu Wawi, wakati akizungumza na wanamichezo kabla ya kuanza kwa michezo ya ligi daraja la pili taifa, mkoa wa kusini Pemba. Alisema ule utamaduni wa kucheza cheza na watoto wa kike na wakati mwengine kuwaita majina kama mchumba, wauwepuke, kwani wapo vijana ambao umeshawawek pabaya, baadhi ya watu. ‘’Kama kuna mtoto wa miaka 12, au 16 hadi 17 umekuwa ukipenda kumtania kwa kumuita mchumba, hili jambo tuwe makini nalo, maana mtoto akidhalilishaji na mtu asiyemju, huwa rahisi kumtaja aliyekaribu naye,’’alieleza. Katika hatua nyingine, Msaidizi huyo wa sheria Jimbo la Wawi Haji Nassor Mohamed, amewaelekeza wanamichezo hao, kuwa kisheria mtoto ni mtu yeyote aliyechini ya miaka 18. ‘’Kwa muji...

CHAPO; WASAIDIZI WA SHERIA CHAPUWENI WIGO WA WANANCHI KUFUATA SHERIA

Image
  NA JUMA SEIF, PEMBA; Wazaidiz wa sheria wametakiwa kuhakikisha wanaisaidia na kuilekeza  jamii katika kutekeleza sheria za nchi. Akizungumza katika mkutano wa jumuiya ya Wasaaidizi wa sheria ya Wilaya ya Chake chake CHAPO uliofanyika Febuari 4, 2023 mjumbe wa bodi wa jumuiya hiyo Kassim Ali Omar amesema wasaidizi wa sheria wanawajibu wa kuiyelekeza jamii katika kuzifahamu na kujuwa namna bora ya kuzitekeleza. Amesema sheria inagusa kila pahala katika maisha ya watu kwani sheria hizo zina lengo la kuleta ustawi na usawa katika maisha ya watu. Mjumbe huyo amesema wasaidizi washeria wanawajibu mkubwa wa kuisadia jamii hasa wakati anapokuwa na tatizo kwqni ndani ya jamii kuna watu wengi wanapokumbwa na tatizo hajui wapi namna ya kuzipata haki zake. "Ni lazima sisi wasaisizi wa sheria tuwape wananchi njia ya kujua haki zao kipinsi wanapokuwa na tatizo, kwani mtu hadi anagika mahakamani anakuwa hajui chochote kuhusu sheria ya kosa lake". Pia Adam Abdalla Fakih ambaye ni mjumbe wa...