Posts

Showing posts from February, 2025

LSF: YATOA USHAURI WA BURE KWA JUMUIYA ZA WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA

Image
  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MRATIBU wa taasisi ya ‘LSF’ kanda ya Zanzibar Hamisa Bakar Hamad, amesema kama jumuiya za wasaidizi wa sheria, hazikuungana wakati zinapotekeleza miradi, inaweza kuwa jambo gumu kufikia malengo ya miradi hiyo kwa jamii. Alisema, jumuiya hizo zote ni zinamalengo yanayofanana ya kuisaidia jamii, hivyo ili kufikia malengo hayo hazinabudi, kushirikishana na kufanyakazi kwa pamoja. Mratibu huyo wa kanda aliyasema hayo, ofisini kwake Madungu mjini Chake chake, kwenye mafunzo ya siku mbili kwa wanaasasi za wasaidizi wa sheria, katika kuutambulisha mradi wa suati ya mwanamke. Alieleza kuwa, kama jumuiya zinaelekea kuisaidia jamii, hakunabudi moja inapotekeleza mradi husika, kushirikiana na nyingine. Alifahamisha kuwa, sio busara kuona taasisi zilizojirani, moja inatekeleza mradi ambao mwenzake alishautekeleza miezi kadhaa iliyopita. ‘’Kwa mfano kama ‘CHAPO’ anatekeleza mradi wa afya ya mama, ni vyema na jirani yake ‘MDIPAO’, kuelekezana ili kusaidiana ushauri na...

IDARA YA KATIBA: ‘’KUJITOLEA KWA WASAIDIZI WA SHERIA NI TAKWA LA KISHERIA’

Image
    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa Divisheni ya Katiba na Sheria Pemba Bakari Omar Ali, amewasisitiza wasaidizi wa sheria, kukumbuka kuwa ,   bado dhana ya kujitolea kwa aina ya kazi yao hiyo, itabakia pale pale licha ya changamoto walizonazo. Alisema, kwa mujibu wa sheria inayowaongoza, ni kosa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria na kisha kuomba malipo kwa m wananchi husika. Mkuu huyo wa Divisheni, aliyasema hayo leo Febuari 9, mwaka 2025  ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ wakati akitoa maoni yake, baada ya kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti kwa wasaidizi wa sheria ,   kisiwani humo. Alisema, ijapokuwa sasa wapo wanaodai malipo kama baraka ya kufanyakazi zao, lakini bado sheria haitambuwi uwepo wa posho kama motisha wa kufanya kazi zao. Alieleza kuwa, msingi mkuu wakati wa lipo omba kazi hiyo na sasa ikiingizwa ndani ya sheria yao, ni kufanyakazi kwa njia ya kutolea, na hasa kwa wananchi wany...