WANANCHI PUJINI WATAJA VYANZO VYA MIGOGORO YA ARDHI
NA HAJI NASSOR, PEMBA WANANCHI wa shehia za Pujini, Mfikiwa na Dodo mkoa wa kusini Pemba, wamesema moja ya sababu inayochangia uwepo wa migogoro ya ardhi katika jamii, ni ucheleweshwaji wa mirathi kwa wahusika. Walisema, wapo baadhi ya wanaume katika familia, mara baada ya kifo cha mrithiwa, huikumbatia mirathi na wakati mwengine hadi kuwapa lugha za vitisho warithi wenzao, na mwisho huzaliwa migogoro inayozuilika. Wakichangia mada ya usuluhishi wa migogoro ya aradhi, kwenye mafunzo ya kuzuia migogoro kwenye maeneo ya uwekezaji na kufanyika kituo cha ubunifu wa kisayansi Pujini, wananchi hao walisema, hilo bado ni tatizo. Walieleza kuwa, wanaume hao wamekuwa wakipuuzia maandikiko matakatifu yanayohimiza suala la kulipa kipaumbele urithi, mara baada ya muhusika kufariki. Mmoja kati ya wananchi hao Abdallah Kombo, alisema utamaduni wa kumilikiwa mirathi na mtu mmoja, na kuwaacha wengine pembeni, huzaa migogoro mfano kama ya ardhi. ‘’Moja ya sababu ya uwepo wa migogoro n...