CHAPO: 'WAPENI ELIMU YA KINGA WAZAZI WIZI WA WATOTO'

 


 NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@

JUMUIYA ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ imewakumbusha wasaidizi wa sheria wilayani humo, kutilia maanani, elimu kwa jamii, juu ya wimbi la wizi wa watoto lililoibuka hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 27, 2024 na Afisa Ufuatiliani na Tathmini kutoka ‘CHAPO’ Wahida Kombo Khamis, kwenye kikao cha mwezi cha kuwasilisha ripoti za elimu na msaada wa kisheria, kilichofanyika ofisini kwao mjini Chake chake.

Alisema, pamoja na kuwaelimisha wananchi juu ya udhalilishaji, migogoro ya ardhi, ndoa, wizi, dawa za kulevya pamoja na kuhubiri amani, lakini watilie mkazo, juu ya elimu ya tahadhari ya wizi wa watoto.



Alieleza kuwa, ijapokuwa kwa wilaya ya Chake chake halijakua la kutisha jambo hilo, kama ilivyo kwa baadhi ya mikoa ya Tanzania bara, lakini ni vyema, kinga ikaanza kuwekwa.

Alifahamisha kuwa, hilo ni miongoni mwa majukumu ya wasaidizi wa sheria, hivyo ni wakati sasa kulieleza kwa upana, ili jamii ifahamu na izidishe ulinzi kwa watoto wao.

‘’Tukianza kutoa elimu kwa jamii, kuanzia mwezi Augost mwaka huu, tusisahau kuwaeleza kwa upana, juu wizi wa watoto, ambao kwa mikoa ya Tanzania limekuwa maarufu,’’alieleza.

Katika hatua nyingine, Afisa huyo Ufuatiliaji na Tathmini Wahida Kombo Khamis, aliwataka wasaidizi hao wa sheria, kuwasilisha mapema ripoti zao za kutoa elimu na msaada wa kisheria.

Mapema Mkurugenzi wa ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, alisema kuanzia sasa, ripoti zote za wasaidizi wa sheria za mwezi, siwasilishwe sio zaidi ya tarehe 3 ya mwezi mpya.



‘’Imekuwa uletaja wa ripoti haupewi kipaumbele, sasa ili kuhakikusha tunakwenda vizuri, kila msaidizi wa sheria, awasilishe ripoti na iwe mwisho wa mwezi husika na sio vyenginevyo,’’alifafanua.

Katika hatua nyingine, aliwataka wasaidizi wa sheria wakongwe, kuzidisha ushirikiano wao wa karibu na wale wapya, ili lengo la kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria, litimie.

Aidha Mkurugenzi huyo, amewakumbusha wasaidizi hao wa sheria, wanapopata mafunzo, kuhakikisha wanakuwa na mrejesho kwa kuwasomesha na wingine.

Mratibu wa CHAPO Mohamed Hassan, aliwakumbusha wasaidizi hao wa sheria, kuendelea kufanya kazi za kuwaelimisha wananchi, juu ya sheria mbali mbali.



Alieleza kuwa, zipo sheria kadhaa zimeshafanyiwa marekebisho na nyingine ni mpya, hivyo ni nafasi yao, kuhakikisha wanawaelisha wananchi katika shehia zao.

Mkurugenzi fedha wa ‘CHAPO’ Riziki Hamad Ali, aliwakumbusha wanachama hao, kuhudhuria katika shughuli zote wanazoalikwa, bila ya kujali nauli.



Masaidizi wa sheria kutoka Wesha Khadija Said Khalfan, alisema ushirikiano ndio njia pekee, utakayofanikisha kazi zao za kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria, kwa jamii.

Msaidizi wa sheria Jimbo la Chonga Asha Hamad Faki, aliwasisitizia wenzake, kuendelea kuwa karibu na wasaidizi wa sheria wapya, ili kuwajenga kiuwezo.





Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ imekuwa na utaratibu wa kukutana na wanachama wake kila mwishoni mwa mwezi, kwa ajili ya kuwasilisha ripoti na kuibua changamoto, zinazokwaza katika shughuli zao.

                  Mwisho    

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’