WATU WENYE ULEMAVU PEMBA: “BADO HAKI ZETU ZINAPIGWA MATEKE’’
NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
WATU
wenye ulemavu kisiwani Pemba, wamesema bado wanamashaka na utekelezaji wa haki
zao, ikiwemo ajira, miundombinu ya kuyafikia majengo ya umma na upatikanaji
huduma za kijamii kwa ina ya mazingira yao.
Walisema,
wamekuwa na watetezi wengi mno katika taifa, lakini kwenye utekezaji halisi,
wanaendelea kukumbana na vikwazo, hali inayosababisha kuwavunja moyo, kwa
baadhi ya wakati.
Hayo waliyasema Novemba 27, 2023 kwenye kongamano la siku moja, lililoandaliwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria
wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ na kufanyika ofisi ya Umoja wa Watu Wenye
Ulemavu ‘UWZ’ Mkanjuni, ikiwa ni muendelezo wa mikutano, ya ndani ya siku 16 za
kupinga ukatili na udhalilishaji.
Walisema, hadi
miaka ya hivi karibuni, yapo majengo ya umma yanajengwa bila ya kuzingatia miundombuni
yao, jambo linalowavunja moyo na kujiona wanatengwa.
Mjumbe wa ‘UWZ’
Nassor Suleiman, alisema wamekuwa wakijuliza kwamba sasa wafike pahala, wasizungumze
jambo lolote wanapotakiwa kutaja changamoto zao, kwa kuhofia kutofanyiwa kazi.
‘’Kwa mfano
hata ujenzi wa soko letu jipya la Machomanne Chake chake, kuna sehemu kubwa
inavizingiti, na hili wakati linajengwa sheria yetu mpya imeshatungwa, sasa
tunajiuliza mbona tunasahauliwa kutekelezewa maoni yetu,’’alieleza.
Mjumbe wa ‘UWZ’
wilaya ya Wete Katija Mbarouk Ali, alisema changamoto kubwa, ni kukosa uhakika
wa kutekelezwa kwa vitendo, juu ya dhana ya ajira kwao wao.
‘’Tunasikia
tu kwamba, watu wenye ulemavu wanatakiwa waajiriwe kwa asilimia kadhaa, lakini
hatuoni jambo hilo, likitekelezwa kwa vitendo, na bahati nzuri sera na sheria
zipo, sasa hapa hatujui tufanye nini,’’alilalamika.
Alieleza kuwa,
changamoto nyingine ni kuweko kwa watendaji katika ofisi za umma za watu wenye
ulemavu, wasiokuwa na ulemavu, jambo linalosababisha kukosekana kwa upokeaji mzuri.
Mjumbe wa Kamati
Tendaji wa Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAUZA’, Hidaya Mjaka
Ali, alisema katika eneo la mahkama bado watu wenye ulemavu na hasa viziwi,
hawajatendewa haki.
‘’Hakuna mkalimani
rasmi katika mahkama zetu, na wakati mwingine hutafutwa lakini hasa kwa kesi za
udhalilishaji pekee, je hizi kesi nyingine haki ya watu kwa kundi hili
inapatikanaje,’’alihoji.
Mwanachama wa
Jumuiya ya watu wenye ulemavu Pemba, Salim Abdalla Salim alisema, pamoja na
juhudi za serikali za kutaka watu wenye ulemavu, wapatiwe haki zao, lakini wapo
wanaokwamisha.
‘’Serikali
imeweka mikakati na sera nzuri, kwa ajili yetu, lakini sasa inatakiwa kila
jambo lisimamiwe kwa dhati, ili kuhakikisha tunapata haki zetu,’’alifafanua.
Akizungumzia
siku 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, alisema ni muhimu
kwao, kutafakari namna wanavyopatiwa haki zao za binaadamu, ikiwemo kushirikishwa.
Mjumbe wa
Jumuiya ya wasioona wilaya ya Mkoani ‘ZANAB’ Halima Suleiman Kombo, aliishauri Tume
ya Utumishi serikalini, kuhakikisha wanaweka mifumo jumuishi, wanapotangaaza
ajira kupitia mitandaoni.
‘’Kama dunia
imefika mbali, wenye taasisi za kutoa ajira, watumie mifumo jumuishi, maana
wako wananchi wanaulemavu wa uoni, sasa mifumo nayo isiwatenge,’’alifafanua.
Akifungua
kongamano hilo, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya wasaidizi
wa sheria Chake chake ‘CHAPO’ Kassim Ali Omar, alisema kongamo hilo, ni jukwaa
kwa watu wenye ulemvu, kueleza changamoto zao.
‘’Watu wenye
ulemavu wanachangamoto kadhaa, na ndio maana CHAPO, ikaamua kukutana na nyinyi,
ili kuzitumia siku 16 hizi za kupinga ukatili na udhalilishaji,’’alieleza.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Mkoani Nassor
Hakim Omar, alisema njia moja ya kupunguza changamoto zinazowakabili watu wenye
ulemavu, ni kuzisemea kila wanapopata nafasi.
‘’Msikae
kimnya kila mnapopata nafasi, changamoto zilizopo mzizungumze, na sisi wadau wa
haki jinai, tunaendelea kushirikiana kila wakati, ili kuhakikisha tunafikia
ndoto zetu,’’alieleza.
Mwakilishili
wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Wete Said Hassan Rashid, alisema
kama nchi haijakuwa na sera maalum na kutekelezwa, changamoto za watu wenye
ulemavu zitazungumzwa bila ya kumalizika.
Mkurugenzi
wa ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali aliwataka viongozi hao wa jumuiya za watu wenye ulemavu,
kushirikiana na wasaidizi wa sheria, ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zao.
‘’Pamoja na
changamoto hizo, lakini sihaba serikali imeweka miundombinu mizuri kwa ajili
yenu, kama kuwepo wa Idara, mikopo na sheria nambari 8 ya mwaka 2022 iliyokuja
kulinda haki zenu,’’alifafanua.
Jumuiya ya
wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake CHAPO, imo katika mikutano yake
kadhaa, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili na
udhalilishaji.
Mwisho
Comments
Post a Comment