CHAPO: ‘WAZAZI TENGENI MUDA KUZUNGUMZA NA WATOTO WENU’
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAZAZI na walezi wa
kijiji ch Jamvini shehia ya Ndagoni, wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kutenga
muda wa kukaa na watoto wao, ili kuwahoji yaliotokezea mchana mzima, kwa lengo kubaini
ikiwa wameanza kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ama laa.
Ushauri huo umetolewa Novemba 25, 2023 na Masaidizi wa sheria Jimbo la Ziwani, shehia ya Wesha Khadija Said Khalfan,
wakati akizungumza na wazazi na walezi, pamoja na watoto wao, wa kijiji cha
Jamvini, ikiwa ni mikutano ya kutoa elimu ndani ya siku 16 za kupinga ukatili
na udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Alisema, njia moja wapo
ya kubaini, iwapo mtoto ameanza kubadili tabia na hasa kwenye vitendo vya udhalilishaji,
ni wazazi kutenda muda, wa kukaa na watoto hao.
Alieleza kuwa,
hipendezi kuona wazazi hao, wanaelekeza nguvu zao zaidi katika kutafuta maisha
pekee, bali waelewa kuwa, sasa ulimwengu umebadilika na yapo majanga ambayo
huwakumba watoto.
Msaidizi huyo wa
sheria, alifafanua kuwa, kupitia mazungumzo ya watoto, wanapokaa na wazazi ama
walezi wao, wanaweza kugundua ikiwa wameanza kutekwa kiakili na wadhalilishaji.
‘’Ni kweli maisha
yamepanda juu, na wapo wazazi wanatoka alfajiri na kurudi nyumbani usiku,
lakini ili kukabiliana na majanga haya, tujitengee muda kukaa na watoto wetu,’’alisisitiza.
Katika hatua
nyingine, Msaidizi huyo wa sheria, alisema wao wapo kwa ajili ya kuwasadia
wananchi, ikiwemo kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria, bila ya malipo.
‘’Mnapoona kuna
kitu kinawatatiza kisheria, tutafuteni ofisi yetu ipo Chake chake mjini mkabala
na tume za uchaguzi, na tunatoa msaada wa kisheria bila ya malipo,’’aliafafanua.
Kuhusu siku16 za
kupinga ukatili na udhalilishaji, aliitaka jamii kila mmoja, kuwa mlinzi kwa
mwenzake, ili kuhakikisha hakuna anayezifanyia sulhu kesi za udhalilishaji.
Kwa upande wake Mkaguzi
Msaidizi wa Polisi anayefanyakazi katika shehia ya Ndagoni na Wesha Khamis Asli
Khamis, aliikumbusha jamii, juu ya wajibu na haki yao ya kushirikiana na vyombo
vya sheria, ikiwa wana nia ya kutokomeza uhalifu.
Alieleza kuwa,
jamii inaweza kushirikiana kwa njia kadhaa ikiwemo ya kutoa ushahidi, kuonesha
mtuhumiwa alipo, kutoa elimu ya athari ya uhalifu pamoja na kuzifikisha kesi
katika vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha askari huyo
shehia, aliwataka watoto kutoa taarifa pindi watakapoona dalili za kutaka
kudhalilishwa hata iwe kwa baba, kaka, mjomba, mwalimu wa skuli au mtu mwingine
wa familia.
‘’Hata kama anayekushika
shika sehemu zako za siri ni mwalimu au kaka, toa taarifa kwa mama au kwa mtu
mwingine unaemjua, ili nae achukuliwe hatua, maana hicho ndio chanzo cha kutaka
kufanyiwa udhalilishaji,’’alieleza.
Nae Mratibu wa
wanawake na watoto shehia ya Ndagoni Shuwarika Ali Mohamed, alisema hatomuhurumia
mtu yeyote, ambae atakua na kesi ya jinai, na kisha kuanza taratibu za kuzisuluhisha.
‘’Ipo tabia kwa
baadhi ya watu, wanaweza kujua mtoto wake amedhalilishwa, basi wakakimbilia
kwenye ufungaji wa ndoa, na wasipofahamiana huko, huja kwangu, kwamba kesi
tuishughulikie lakini nasema naanza na wewe kwanza kukuripoti sehemu husika,’’alieleza.
Hata hivyo,
amewakumbusha wananchi kuendelea kuwatumia wasaidizi wa sheria, kwani wana
nafasi kubwa katika suala la kuelimisha jamii, juu ya umuhimu wa kuzilinda haki
za binaadamu.
ia ya wasadizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba CHAPO, imo katika kampeni maalum ya kutoa elimu ya kupinga ukatili na udhalilishaji, ndani ya siku 16 za kupinga ukatili, kwa kupita katika shehia mbali mbali za wilaya hiyo.
MWISHO



Comments
Post a Comment