CHAPO: ‘’WANAFUNZI JIEPUSHENI KUFANYIANA UDHALILISHAJI WENYEWE’’

 


NA ASHA ABDALLA, PEMBA

WANAFUNZI wa Almadrassatul-nurul- huda ya kijiji cha Mjengo wa Banda shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kuepukana na kufanyiana vitendo vya udhalilishaji miongoni mwao, kwani madhara yake ni makubwa.

 Hayo yameelezwa leo Novemba 12, 2023 na Msaidizi washeria  wa jimbo la Wawi, Haji Nassor Mohamed, wakati alipokua akitoa taaluma katika madrassa hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji mpango kazi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba CHAPO.

Alisema zipo njia mbalimbali ambazo mtu humfanyia mwenzake kumpelekea kumuathiri kiakili, kimwili na kijamii ikiwemo kumwita jina baya au kumpiga kipigo cha kuathiri mwili wake.

Alisema, zipo aina nyingi za udhalilishaji lakini ambazo hazizungumzwi sana ni kuitana majina mabaya, kuzomeana, kuigizana na kwa sauti au Watoto wenyewe kwa wenyewe kudhalilishaana kingono.

‘’Zipo tabia mbali mbali kwa wanafunzi hasa wakike, yakupigana makofi sehemu za makalio au kwenye kifua, na kwaupande wanafunzi wanaume kufanyiana michezo ya kwenye vichaka, na kisha kulipiziana kwa mfumo wa kudhalilishana,’’alieleza.

Akizungumzia kuhusu njia chafu ambazo mtoto anaweza kukubali kudhalilishwa ni kwa baadhi ya wazazi na walezi, kuwaachia watoto wao kuangali michezo kwenye tv au kuchezea simu zao na kuona picha zilizo nje ya maadili yao.

‘’Katika baadhi ya nyumba wazazi wanadhani kuwapenda watoto wao, ni kuwaachia tv na kuweka michezo watakayo, bila ya kujali athari ya wanachokiangalia,’’alifafanua.



Hata hivyo, amewakumbusha kuwa, wanapoona wenzao au wao wenyewe kuna viashiria vya kutaka kufanyiwa vitendo vya udhalilisaji, wasisite kutoa taarifa aidha kwa waalimu, wazazi, walezi au uongozi wa sheria.

Kwa upande wa Mwanafunzi wa madrasa hiyo Rufaida Abdalla Omar, alitaka kujua kuhusu wanawake kwa wanawake, kupigana mabusu bila yamwenyewe kuridhiana, ikiwa hilo ni kosa kisheria.

 Nae mwanafunzi Hashiri Kombo Hamad, alitaka kujua kutoka kwa Msaidizi huyo wa sheria, juu ya suala ka kuchungulia ndani  mwa mtu (kupiga bodi), ikiwa linaingia katika makosa ya udhalilishaji.

‘’Maana wapo watu wanapiga bodi katika nyumba za watu, lakini sioni wakichukuliwa hatua, na je hili nalo ni kosa katika yale ya udhalilishaji,’’aliuliza mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mwanafunzi Nihlat Mohamed Abass, alita kuwepo kwa muongozo maalumu, kwa waalimu wa madrssa juu ya idadi ya bakora kwa wanafunzi kwa aina ya kosa alilotenda.

‘’Isiwe mwalimu anaamua yeye mwenyewe, juu ya idadai, sasa ni vyema kuwepo kwa muongozo husika wa waalimu juu ya adabu hiyo kwa wanafunzi wao,’’alieleza.

Nae mwalimu mkuu msaidizi namba mbili wa madrasa hiyo  sheikh Juma Khamis Ali, alisema mpango wa serikarekali wa kuanzisha wasaidizi wa sheria, unaleta tija kwa jamii.




Alieleza kuwa, elimu iliyotolewa katika madarassa yake, ni mzuri na imekuja wakati mwafaka, kwani vitendo hivyo vipo kwa wingi katika jamii yao.

Kwa upande wake Mkuu wa madrassa hiyo sheikh Mohamed Omar Mohamed, alisema elimu kama hiyo inafaa kuendelezwa kila baada ya muda, ili watoto wazinduke.

‘’Hapa madrassa wanaelimishwa kila baada ya muda, lakini tukipata na wasaidizi wa sheria wakipita, huwa inatusaidia sisi ulezi,’’alieleza.





Aidha aliitaka CHAPO, kuendelea kuzitembelea madrassa nyingine, ili kukutana na watoto hao na kuwapa elimu kama waliyopewa wao.

Mdarassa hiyo iliyoanzishwa na marehemu mwalimu Abass  Hamad Mjaku mwaka 1980, ikiwa na awanafunzi 20, ambapo kwa sasa ina waalimu watatu, na wanafunzi 130, wakiwemo  wanaume 70 na wanawake 60.

                                              Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’