LFS, YAWAONESHA NJIA MAAFISA MAWASILIANO WA JUMUIYA ZA WASAIDIZI WA SHERIA

 



NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

MAAFISA mawasiliano na habari wa Jumuia za wasaidizi wa sheria Tanzania zimetakiwa kujenga ushirikiano wa karibu na watendaji wenzao, ili kuhakikisha wanakuwa na mifumo sahihi ya utoaji wa taarifa za jumuia.

Hayo yameelezwa Novemva 24, 2023 na Mtaalamu wa masoko kutoka LSF     Gilsant Mlaseko, wakati akizungumza na maafisa  hao kwenye mkutano wa kujengewa uwezo kwa njia ya kielektroniki.

Alisema bidhaa ya mwasiliano sio haki ya Afisa Mawasiliano na Habari pekee kwenye jumuiya, bali anatakiwa kuwa karibu na wakurugenzi, waratibu na watendaji wengine.

Alieleza kuwa, wakati mwingine ndani ya Jumuiya Afisa huyo anaweza kuwa mwisho katika utoaji wa taarifa na hasa baada ya kuidhinishwa na kuthibitishwa na kamati iliyoteuliwa.

‘’Suala la mawasiliano hasa ya kutoka nje ya Jumuiya, linapaswa watoa taarifa wawe makini na sio jukumu la mtendaji mmoja, bali iwe ni timu ya Jumuiya na kisha muhusika anateuliwa,’’alieleza.

Akieleza umuhimu wa mawasiliano Mtaalamu huyo, alisema ni kuwaonesha wananchi kazi zinazofanywa na Jumuiya, kujenga mustakbali  na mwelekeo wa Jumjuiya pamoja na kuonesha kazi zenu.

‘’Wakati mwingine mawasiliano lazima yaangalie kundi la watu fulani, wakati, aina ya lugha, njia za kuwasiliano nao, eneo husika pamoja na kuhakikisha kupata mrejesho hapo  baadae,’’alieleza.

Katika hatua nyingine, amwakumbusha Maafisa hao mawasiliano na habari kuwa wanaweza kutumia nji za mawasiliaono kama vile kuandika, kurikodi sauti na picha, vipeperushi, mabango, ujumbe mfupi na picha pekee.

Aidha aliwaeleza maafisa hao mawasiliano na habari, kuwa wanaweza kuitumia mitandao ya kijamii, kuwasilisha taarifa na maelezo yao, kwa jamii ili kupata taarifa kwa haraka.

Aliwanasihi kuwa, katika eneo hilo ni vyema wakawa makini na kujiridhisha kabla ya kuweka taarifa zao, kwani faida yake kubwa ni kuwafikia wengi kwa muda mfupi na ikitokeza kuna mkanganyiko wa taarifa huwafikia wengi.

‘’Mawasiliano ya haraka moja ni eneo la mitandao ya kijamii, iwe face book, twita, Instagram n ahata tovuti na blog, ingawa athari yake kama hakuna taarifa rasmi au ukikosea huwa shida kurudi kwa wafuatiliaji wako,’’alifafanu.

Akijibu baadhi ya mawasiliano, mtendaji wa LSF Victoria Mshana, alizishauri taasisi ziweke utaratibu wa maandishi kutoa taarifa ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi mbali mbali.

Aidha lisema wawe makini namna ya kuchagua majukwaa ya kutoa taarifa na kufikisha ujumbe mahasusi kwa walengwa wa kundi fulani ndani ya jamii au taifa kwa ujumla.

Mmoja wa washiriki hao Abass Famau, alisema mawasiliano ndio kiungo muhimu na cha lazima kwa taasisi kuhakikisha wanakuwa makini wanapowasiliana na wananchi mbali mbali.

‘’Inawezekana kila mmoja anataka aonekane kwenye vyombo vya habari, hivyo mwingine akazungumza hivi na mwingine akazungumza tofauti na mwenzake, na taasisi ikatafsiriwa vyenginevyo,’’alieleza.

Nao Abass Yussuf Makamba, Bahati Issa Jecha na mwenzake Augusta Chasi wamesema, changamoto inayojitokeza ni kwa baadhi ya wakati kutokuwepo kwa mawasiliano na Internet na kusababisha uzoroteshaji wa mawasiliano.

Akiwasilisha kazi za vikundi Shaabani Chande, amesema mafunzo hayo ni muhimu mno kwao, kwani kwa sasa hakuna mtiririko mzuri wa mawasiliano kuanzia ndani ya shirika hadi nje.

Nae Augustino Chipamba, wameomba mafunzo hayo yawe mara kwa mara na kuhakikisha yanakuwa ana kwa ana, ili ufanisi zaidi upatikane kupitia mafunzo hayo.

Kwa upande wake Saleh Juma, alifafanua kuwa mawasiliani ya kielektroniki yanasaidia kuwaunganisha na wafadhili waliono nje sambamba na mafunzo hayo kufanyika kwa njia ya ana kwa ana.

Akiwasilisha mada ya adabu na maadili katika mawasiliano, Afisa Kujengea Uwezo wa Shirika la Legal Service Facility LSF Victoria Mshana, amesema mawasiliano yenye heshima, nidhamu na adabu ni muhimu kwa pande zote.

                                       Mwisho  

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’