WANAFUNZI 300 WAFIKIWA NA ELIMU YA HEIDH SALAMA PEMBA
AMINA AHMED, PEMBA.
JUMLA ya wanafunzi wakike 300 wa Skuli za Sekondari Msuka na Chambani Kisiwani Pemba wamepatiwa Elimu juu ya mafunzo ya Hedhi Salama, Ukatili wa kijinsia, pamoja na haki ya Hedhi salama kwa Mwanafunzi wa Kike.
Wanafunzi 233 kati ya hao wamepatiwa taulo za Kike zenye uwezo wa kudumu miaka miwili kutoka ikiwa ni shamra shamra za kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 Mwezi wa 3 Duniani kote.
Msaada wa taulo hizo kwa Wanafunzi hao uliotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Smile for Community ni katika utekelezaji wa Mradi wake wa Run for Binti Marathon, ambao umefadhiliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria Legal Services Facility unaotekelezwa kwa LSF na kufanya kazi kwa kushirikana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto , Maisha Bora Faundation ZMBF, Taasisi ya Weza, pmojana Taasisi ya Waja Mama.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumaliza kutoa Elimu kwa Wanafunzi hao Afisa Mradi kutoka Shirika la Smile For Community Anet Kiao alisema kuwa lengo la kutoa Elimu juu ya suala hilo ni kuhakikisha Wanafunzi wakike waliopo Maskulini wanakuwa salama wanapokuwa katika kipindi cha Hedhi.
Alisema suala hilo litawafanya Wanafunzi wa kike kuendelea vyema na Masomo bila kupata usumbufu utakaowapelekea kushindwa kufanya vizuri katika Masomo yao na badala yake waweze kuedelea kubaki skuli kuendelea na Masomo yao.
"Lengo la kugawa Taulo hizi kwa wanafunzi wakike ambao wameshafikia umri wa balehe ni kuona wanaondokana na usumbufu wanaokumbana nao wakati wa Hedhi, pale wanapokuwa Skuli ambao kwa namna moja ama nyengine hupelekea kukatisha Masomo yao au kushindwa kufanya vizuri Darasani wanapokuwa katika hali hiyo kupitia Elimu hii tuliyoitoa kwa wanafunzi hawa watajua sasa nini wafanye wanapokumbana na suala hili", alisema.
Akitoa Elimu ya Kisheria kwa Wanafunzi hao Alphonce Mbarambe Gura Mwanasheria kutoka taasisi ya Legal Service Facility Zanzibar aliwataka Wanafunzi hao kutokaa kimya wanapokumbana na changamoto yeyote inayotokana na Hedhi kwa vile suala hilo linatambulikana kikatiba kama ni haki ya Msingi kati ya Haki za Binaadamu kwa vile suala hilo linagusa moja kwa moja utu wa Wanafunzi hao wakike.
"Lazima suala la Hedhi Salama liangaliwe kwa upana wake hivyo ni lazima Watoto wakike wenyewe muweze kujua ni jinsi gani suala la hedhi Salama ni muhimu kwenu, mna haki ya kupata vifaa vya kujisitiri kwa gharama nafuu ambavyo ni salama , kupata Mazingira wezeshi Skuli na Nyumbani ya kubadilishia nguo maji ya Salam kwa vyovyote hivi munahaki ya kudai endapo mtakuwa Skuli ama Majumbani", alieleza.
Nao baadhi ya Wanafunzi waliopatiwa Elimu juu ya masuala hayo akiwemo Fatma Abdalla Mbarouk kutoka Skuli ya Msuka Sekondari pamoja na Ruwaida Salum Hamad waliwashukuru Wafadhili hao waliojitolea kuwafikishia Elimu hiyo ambapo walisema itawasaidia katika kukabiliana na changamoti ambazo walikuwa wanakumbana nazo awali kabla ya kupata Elimu hiyo.
"Tunaahidi kuifanyia kazi Elimu hii ili isiwe kikwazo tena kwetu kupata changamoto zinazopelekea kuwa watoro tunapokuwa katika Hedhi ",Alisema Fatma Abdalla Mbarouk.
Waliyaomba na Mashirika mengine pamoja na taasisi mbali mbali waige mfano huo mzuri ambao utasaidia kufanikisha malengo ya Wanawake waliyojiwekea kwani bado Elimu hiyi na Taulo hizo wapo wanafunzi wengi ambao wanazihitaji katika skuli nyengine .
Elimu iliyotolewa kwa wanafunzi hao ni pamoja na namna ya kujikinga na kutambua viashiria vya Ukatili wa kijinsia, matumizi salama ya Taulo za kike za kufua, pamoja na haki ya Kisheria ya Afya ya Hedhi Salama kwa Wanafunzi wa kike Maskulini ikiwa ni shamra shamra za kuelekea siku ya Wanawake Duniani ambapo ugawaji wa Taulo hizo zimepatikana kupitia kupitia Kampeni ya Twende pamoja Run for Binti Marathon.
.jpg)
.jpg)

Comments
Post a Comment