..........FUATILIENI MABADILIKO YA SHERIA MSIJEWAPOTOSHA WANANCHI
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WASAIDIZI wa sheria nchini,
wameshauriwa kuwa wafuatiliaji na kujisomea zaidi, ili kujua mabadiliko ya
sheria, ili kuwarahisishia wanapokwenda kwa wananchi kutoa elimu.
Ushauri huo
umetolewa Machi 30, 2023 na Afisa wa Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar
Ali Haji Hassan, wakati akiwasilisha mabadiliko ya sheria, ikiwemo ya Ushahidi
nambari 9 ya mwaka 2016, kwenye mafunzo kwa njia ya zoom kwa wasaidizi wa
sheria.
Alisema,
moja ya jukumu la msaidizi wa sheria ni kufuatilia kwenye mamla husika, ili
kujua ikiwa kuna mabadiliko ya aina yoyote, ili yamsaidie katika utoaji wake wa
elimu kwa jamii.
‘’Sisi
wasaidizi wa sheria na wengine, tuweni makini kila wakati ili kutambua ikiwa kuna
mabadiliko ya sheria au matamko mengine, ili tuwalishe wananchi chakula halali,’’alisisitiza.
Akizungumzia
mabadiliko ya sheria ya ushahidi iliyokuwa ya mwaka 1917 na kupatikana kwa
sheria nambari 9 ya mwaka 2016, alisema imekuja kuweka mazingira mazuri kwa
mashahidi.
‘’Sheria hii
sasa imekuja kuweka ulinzi maalum kwa mashahidi, lakini pia imekuja kuutambua
ushahidi wa mtoto, ushahidi wa kielektroniki ukiwemo wa picha na sauti,’’alielza.
Kuhusu mabadiliko
ya sheria Mahakama ya Ardhi nambari 7 ya mwaka 1994 kama ilivyorekebishwa kuwa
nambari 1 ya mwaka 2008, alisema imekuja kuondosha baadhi ya changamoto.
‘Moja ambalo
limekuja ndani ya sheria hii ni Mwenyekiti wa mahakama hiyo, sasa rais kaba ya
kumteua sheria imemlazimisha, ashauriane na Jaji Mkuu,’’alieleza.
Aidha
alisema jengine lilomo kwenye sheria hiyo mpya ni Mwenyekiti huyo kutambuliwa
kwa saifa ya shahada ya kwanaza ya sheria.
Kwa upande
wake Afisa sheria kutoka Idara hiyo Salma Suleiman, akiwasilisha mabadiliko ya
sheria ya watu wenye ulemavu ya nambari 8 ya mwaka 2022, alisema imekuja
kuelekeza makosa mbali mbali.
‘’Kwa mfano
yametajwa makosa ya kumuigizia kwa sauti, mwendo, kumdharau, kumkebehi,
kumfungia ndani na kumbagua, ambapo baadhi yao hayakuwemo kwenye sheria kongwe
ya nambari 9 ya mwaka 2006,’’alieleza.
Aidha Afisa
huyo alieleza kuwa, ni wakati sasa kwa wasaidizi wa sheria kuchukua juhudi za
maksudi za kuzitambua sheria kongwe na mpya, ili iwe rahisi wanapotoa elimu kwa
jamii.
Afisa kutoka
taasisi ya LSF Alphonce Marandu, alisema wasaidizi wa sheria wamekuwa kimbilio
kubwa kwa jamii, hivyo lazima wajiendeleze.
Khamis Faki
kutoka Jumuia ya wasaidizi wa sheria Wete, alisema elimu zaidi inahitaji kila
siku kwa jamii, katika kushirikiana na wasiaidizi wa sheria.
Akizungumza nje
ya mkutano huo, Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake
chake Pemba ‘CHAPO’ Nasor Bilali Ali, alisema jambo linalofanywa na LSF na
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria, ni jema.
‘’Mafunzo ya kukumbushwa sheria mpya zilizofanyiwa marekebisho na nyingine kufutwa ni jambo jema, maan sisi wasaidizi wa sheria ndio ambao tunakwenda kwa jamii kila siku,’’alifafanua.
Mafunzo ni
muendelezo wa ushirikiano kati ya LSF na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria
Zanzibar, katika kuwaendeleza na kuwaongezea maarifa wasaidizi wa sheria.
Mwisho


Comments
Post a Comment