MKURUGENZI CHAPO, AWAPA USHAURI WA BURE MASHEHA
IMEANDIKWA NA KHADIJA NA HAJI- CHAPO:::
MKURUGENZI
wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheri wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Nassor
Bilali Ali, amewataka masheha, kutayarisha kamati za usuluhishi wa migigoro ya
ardhi, zinazokubalika na jamii, ili iwe rahisi wakati wa utendaji wao wa kazi.
Alisema, moja ya jukumu la kamati hizo hapo baadae, ni kusikiliza
migogoro ya ardhi, na kuota ushauri kwa ajili ya kupatikana kwa sulhu, hivyo
lazima wachugue wajumbe wanaokubalika katika jamii.
Ushauri huo, ameutoa jana wakati akizungumza, kwenye uzinduzi wa mradi
wa Kujenga uwelewa kwa jamii, katika kuzuia migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi
ya uwekezaji, na kufanyika skuli ya Pujini wilaya ya Chake chake.
Alisema, kamati hiyo itaundwa na wajumbe, na kisha kupewa elimu ya
utatuzi wa migogoro na hata baada ya mradi huo kukamilika, itatakiwa kuendelea
kufanyakazi kwa jamii.
‘’Masheha ni watu wenye uwelewa mkubwa, hivyo natamani sana kuona
wakati ukifika, tupate wajumbe wa kamati wanaokubalika ndani ya jamii,’’alishauri.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa CHAPO, alisema pamoja na
uwepo wa wasaidizi wa sheria karibu kila shehia, lakini CHAPO, iliona vyema
kutafuta mradi huo, ili kuwafikia wananchi wengi kielimu.
Mapema akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, sheha wa shehia ya
Pujini Khamis Uledi Kombo, aliishukuru CHAPO, kwa uamuzi wake wa kuendesha
mradi huo katika shehia yake.
Akieleza malengo la mradi huo, Mratibu wa mradi kutoka ‘CHAPO’ Riziki
Hamad Ali, alisema mradi huo wa mwezi mmoja, utakuwa na shughuli tatu kuu, ikiwemo
mafunzo ya utatuzi wa migogoro kwa masheh, wajumbe wao na wasaidizi wa sheria.
‘’Shughuli nyingine itakayofanyika ni kuunda mabaraza ya shehia ya
usuluhishi wa migogoro na mikutano ya wazi kwa wananchi, ambayo watapata fursa
ya elimu,’’alifafanua.
‘’Sisi pamoja na wafadhili wetu ‘foundation’ tunatarajia baada ya
kumalizika kwa mradi huu, kwanza migogoro ya ardhi ipungue na vijana wahamasike
kutunza amani na kudumu kwa baraza ya usuluhishi,’’alieleza.
Akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro, mtoa mada Mohamed Hassan
Abdalla, alisema elimu ndogo ya sheria za ardhi, ni moja ya sababu za uwepo wa
migogoro ya ardhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya
Mkoani Nassor Hakim Haji, alisema moja ya faida ya mabaraza ya usuluhishi wa
migogoro ni kupunguza kesi mahakamani.
Wakichangia kwenye mkutano huo, washiriki hao walisema mradi huo ni mzuri, maana unaweza kuwa chachu ya kupungumza migogoro ya radhi.
Sheha wa shehia ya Mfikiwa Bimkubwa Tangwi, alisema jamii imekuwa
ikisababisha migogoro ya aradhi, kutokana na kutokujua sheria husika.
Nao washiriki Salim Ali Matta, Abeda Adi Seif, Idrissa Khamis Vuai na
Thuheni Talib Thuheni, walisema licha ya muda mfupi wa mradi huo, lakini kama
mabaraza yatakayoundwa yatafanyakazi kwa bidii, migogoro ya ardhi itapungua.
Shehia ambazo zinatekeleza mradi huo ni Pujini, Dodo na Mfikiwa,
ambapo wajumbe wanne na sheha kila shehia walihudhuria kwenye uzinduzi wa mradi
huo.
Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake CHAPO ambayo
imeanzishwa mwaka 2016, moja ya majukumu yake ni kutoa elimu, ushauri na msaada
wa kisheria bila ya malipo kwa wananchi.
Mwisho


.jpg)






Comments
Post a Comment