CHAPO, FUNDATION LEO PUJINI KUZINDUA MRADI WA KUZUIA MIGOGORO YA ARDHI

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA

JUMUIYA ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ leo Julai 23, mwaka huu, inatarajia kuzindua mradi wa mwezi mmoja wa ‘Kujenga uwelewa kwa jamii katika kuzuia migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi, kwa shuguli za uwekezaji Pemba.

Mradi huo ambao unatarajiwa kumalizika Augosti 30, mwaka huu, unatarajiwa kutekelezwa katika shehia tatu za Mfikiwa, Pujini na Dodo ukifadhiliwa na tasisi ya ‘the foundation for Civil Society ya Tanzania’.

Akitoa taarifa ya namna ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya watendaji wa CHAPO, kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwao Chake chake, Mkurugenzi wa ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali, alisema upatikanaji wa mradi huo, ni faraja kwao.

Alisema, ni sahihi katika maeneo yenye uwekezaji suala la uwepo wa migogoro ya ardhi, baina ya wananchi na wawekezaji huwa haliepukiki, na ndio maana wametafuta mradi huo.

Alieleza kuwa, CHAPO kwa kushirikiana na wafadhili wao, watakuwa na mikutano miwili ya ndani, na mikutano mitatu ya wazi kwa jamii za shehia hiyo.

‘’Mkutano unaotarajiwa kufanyika Julai 23, skuli ya Pujini utahusisha wanajamii 15 wakiwemo masheha na wasaidizi wa sheria 12, lengo na kuutangaza mradi huo, pamoja na kuona hali halisi ya ufahamu wa wananchi,’’alieleza.

Katika hatua nyingine Mkurugenzu huyo, amewataka watendaji wa ‘CHAPO’ kujipanga vyema, ili kuhakikisha wanautekeleza vyema mradi huo, na kwa ufanisi.

‘’Moja ya jukumu la ‘CHAPO’ ni kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na migogoro kama ya ardhi kwa jamii, lakini sasa baada ya wenzetu wa foundation kutuunga mkoano, lazima na sisi tusimame wima,’’alisisitiza.

Mratibu wa mradi huo Riziki Hamad Ali, alisema kilichobakia kwa watendaji wa ‘CHAPO’ kwa watakaobahatika kupata elimu hiyo, ni kuisambaaza katika maeneo mengine.



Alieleza kuwa, kila msaidizi wa sheria ana wajibu wa kuhakikisha jamii iliyomzungumka, inapata uwelewe japo mdogo, ya namna ya kujiepusha a migogoro ya ardhi, iwe kwa mwekezaji au serikali kuu.

‘’Mradi huu ni wa muda mdogo, lakini sisi kama wasiaidizi wa sheria, baada ya kumalizika tuendelee na kazi ya kuisaidia jamii katika kujitenga na migogoro ya aradhi au kuitatua,’’alifafanua.

Nao Mohamed Hassan Ali pamoja na Abeda Adi Seif waliipongeza foundation, kwa kuamua kuichagua ‘CHAPO’ na kuwaamini katika utekelezaji wa mradi huo.



Zaidi ya tasisi tisa zimepata ufadhili wa utekelezaji wa mradi huo, wa mwezi mmoja, wenye wastani wa shilingi milioni 11.

                     Mwisho          

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’