CHAPO YATAMBULISHA MRADI KWA WATENDAJI WAKE
NA HAJI NASSOR, PEMBA
JUMUIYA ya Wasaidizi wa sheria wilaya
ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Julai 23, mwaka huu, inatarajia kuzindua mradi wa
mwezi mmoja wa ‘Kujenga uwelewa kwa jamii katika kuzuia migogoro itokanayo na
matumizi ya ardhi, kwa shuguli za uwekezaji Pemba.
Mradi huo ambao
unatarajiwa kumalizika Augosti 30, mwaka huu, unatarajiwa kutekelezwa katika
shehia tatu za Mfikiwa, Pujini na Dodo ukifadhiliwa na tasisi ya ‘the foundation
for Civil Society ya Tanzania’.
Akitoa taarifa
ya namna ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya watendaji wa CHAPO, kwenye kikao
kilichofanyika ofisini kwao Chake chake, Mkurugenzi wa ‘CHAPO’ Nassor Bilali
Ali, alisema upatikanaji wa mradi huo, ni faraja kwao.
Alisema, ni
sahihi katika maeneo yenye uwekezaji suala la uwepo wa migogoro ya ardhi, baina
ya wananchi na wawekezaji huwa haliepukiki, na ndio maana wametafuta mradi huo.
Alieleza kuwa,
CHAPO kwa kushirikiana na wafadhili wao, watakuwa na mikutano miwili ya ndani,
na mikutano mitatu ya wazi kwa jamii za shehia hiyo.
‘’Mkutano
unaotarajiwa kufanyika Julai 23, skuli ya Pujini utahusisha wanajamii 15 wakiwemo
masheha na wasaidizi wa sheria 12, lengo na kuutangaza mradi huo, pamoja na
kuona hali halisi ya ufahamu wa wananchi,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine Mkurugenzu huyo, amewataka watendaji wa ‘CHAPO’ kujipanga vyema, ili
kuhakikisha wanautekeleza vyema mradi huo, na kwa ufanisi.
‘’Moja ya
jukumu la ‘CHAPO’ ni kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na migogoro kama ya
ardhi kwa jamii, lakini sasa baada ya wenzetu wa foundation kutuunga mkoano,
lazima na sisi tusimame wima,’’alisisitiza.
Mratibu wa
mradi huo Riziki Hamad Ali, alisema kilichobakia kwa watendaji wa ‘CHAPO’ kwa
watakaobahatika kupata elimu hiyo, ni kuisambaaza katika maeneo mengine.
Alieleza kuwa,
kila msaidizi wa sheria ana wajibu wa kuhakikisha jamii iliyomzungumka, inapata
uwelewe japo mdogo, ya namna ya kujiepusha a migogoro ya ardhi, iwe kwa
mwekezaji au serikali kuu.
‘’Mradi huu
ni wa muda mdogo, lakini sisi kama wasiaidizi wa sheria, baada ya kumalizika
tuendelee na kazi ya kuisaidia jamii katika kujitenga na migogoro ya aradhi au
kuitatua,’’alifafanua.
Nao Mohamed
Hassan Ali pamoja na Abeda Adi Seif waliipongeza foundation, kwa kuamua
kuichagua ‘CHAPO’ na kuwaamini katika utekelezaji wa mradi huo.
Zaidi ya
tasisi tisa zimepata ufadhili wa utekelezaji wa mradi huo, wa mwezi mmoja,
wenye wastani wa shilingi milioni 11.
Mwisho




Comments
Post a Comment