MRAJISI WA NGOs: ‘ZAPONET’ JIPANGENI KUJITEGEMEA WENYEWE
MRAJISI wa asasi za kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla, amesema
mtandao wa wasaidizi wa sheria Zanzibar ‘ZAPONET’ ianze sasa kujipanga vyema
kuhakikisha wanajiendesha wenyewe, na sio kutegemea wafadhili.
Mrajisi
huyo aliyasema hayo leo Januari 25, 2026 ukumbi wa Malaria
Mwanakwerekwe Unguja, wakati akiufungua mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka ‘ZAPONET’,
uliokuwa na malengo kadhaa, ikiwemo mapatio ya katiba na uwasilishaji wa ripoti
za wanachama wao.
Alisema,
ZAPONET ni muhimili muhimu kwa jumuia za wasaidizi wa sheria, lakini kikubwa
kwa sasa ni kujipanga mapema, ili kujiendesha yenyewe na kutoa usaidizi kwa wanachama
wao.
Alifafanua
kuwa, ingawa kwa sasa wanaendelea kushikwa mkono na taasisi ya LSF, na kufanya
vizuri katika utendaji wao wa kazi.
‘’Lazima
niwapongeze sana wenzetu wa ‘LSF’ katika kuushika mkono mtandao wa ZAPONET, na
kuwaomba kufanya hivyo, kwani wanufaika wakubwa ni jamii hasa wanyonge,’’alifafanua.
Katika
hatua nyingine Mrajisi huyo, aliwataka viongozi wa ZAPONET kuendelea kushirikiana
kwa karibu na jumuia zote 11 za wasaidizi wa sheria za Unguja na Pemba, ili
jamii iendelee kunufaika na msaada wa kisheria.
Hata hivyo,
aliziagiza jumuia za wasaidizi wa sheria, kuwa na mpango kazi ngazi ya shehia,
katika kutoa elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa wananchi.
Hata hivyo,
aliahidi kuendelea kuwa karibu na ‘ZAPONET’, ili kutatua baadhi ya changamoto
zinazowakabili, ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.
Wakati
huo huo, alizipongeza asasi za kirai Zanzibar, kwa kuhubiri amani na
mshikamano, kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2025.
Mapema
Mwenyekiti wa ‘ZAPONET’ Nassor Hakim Haji, alisema uwepo wa mtandao huo, ni
faraja kwa jumuiya hizo, kwani sasa wamekuwa na mfumo wa sauti moja.
Alifahamisha,
jumuia hizo ambazo nyingi zao zimeanzishwa mwaka 2016, zilikuwa hazina pakukimbilia
wanapokuwa na changamoto zao, ingawa uwepo wa ‘ZAPONET’ sasa kama zimezaliwa
upya.
‘’ZAPONET
ni mkombozi wa jumuiya za wasaidizi wa sheria za Unguja na Pemba, maana dira
yetu ni kuwa chombo cha kuwaunganisha na kuwaweka pamoja wasaidizi wa sheria
wote wa Zanzibar,’’alifafanua.
Aidha kuwa
mkutani huo mkuu wa kwanza, pamoja na mambo mingine utaipitia na kuifanyia
marekebisho katiba ya ZAPONET ili iwe na miundombiu rafiki.
Mwakilishi
mwandamizi wa taasisi ya LSF amesema kwa Tanzania yote, wanafanyakazi na jumuia
za wasaidizi wa sheria 184, ambapo kati ya hizo zipo 30 kwa Tanznania zilipoingia
kwenye mradi huo wa majaribio na mbili zikiwa ni kutoka Zanzibar.
Alisema,
kupitia mradi huo, wametengeneza fungu ambalo litaipa nguvu ZAPONET ili ifanyekazi
zake kwa ufanisi, tokea kuanzishwa kwake mwaka 2019.
‘’Kwa
Zanzibar zipo jumuiya ya wasaidizi wa sheria ya wilaya ya Kaskazini ‘A’ NAPAC
na jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Micheweni ‘MDIPAO’ ambao ndio
wanaoendesha mradi wa ‘Sauti ya mwanamke’ kwa majaribio,’’alifafanua.
Hata hivyo
alisema anatamani kuona siku moja, jumuiya za wasaidizi wa sheria, inajiendesha
wenyewe kuanzia vifaa, majengo na rasilimali fedha.
Akiwasilisha
ripoti ya utendaji kazi, Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya
Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Mohamed Hassan Abdalla, alisema kwa upande wa elimu
waliwafikia wananchi 25,972, wakiwemo wanawake 11,741, wanaume 12,462, watoto
1474 na watu wenye ulemavu 294.
Kwa upande
wake Asia Fadhil Makame kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya
Kaskazini ‘A’ NAPAC alisema, bado changamoto ni kuongezeka kwa matendo ya
udhalilishaji ndani ya jamii.
Mwisho
Comments
Post a Comment