SHEHIA YA MVUMONI WAZINDUA KAMATI YA KUPINGA UDHALILISHAJI
NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MKUU wa Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii Pemba, Omar Mohamed Ali
amesema kuwa kuundwa kwa kamati ya kupinga na kupambana na vitendo vya
udhalilishaji, itasaidia kwa kiasi kikubwa, kuandaa jamii yenye ustawi bora
ambayo itawaweka wanawake na watoto, katika mazingira yaliyosalama.
Alisema kuwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, bado
vinaendelela kujitokeza katika jami, hivyo serikali, inaendelea kutumia mbinu
tofauti, ikiwemo kuunda kamati za shehia, wilaya, mkoa na taifa, ili kupambana
na na vitendo hivyo.
Aliyasema hayo katika uzinduzi wa kamati ya kupinga udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto shehia ya Mvumoni, hafla iliyofanyika skuli ya sekondari ya Furaha.
Alieleza kuwa, kuwepo kwa vitendo hivyo vimekuwa vikiwarudisha nyuma, baadhi ya jamii kwa kuona muhali wa kuviripoti, hivyo uwepo wa kamati hiyo inaweza kuwa mwarubaini.
"Nendeni mkafanye kazi kwa kuielimisha jamii, juu ya athari ya vitendo vya
ukatili na udhalilishaji wa kijinsia pamoja na kuondosha muhali wa kuvinyamzia
kimya, ili kupata ustawi ulio bora na kuwaweka wanawake na watoto, katika
mazingiara yaliyosalama.
Mkuu huyo ameitaka kamati hiyo kutokatishwa tamaa na baadhi ya watu, kwenda
kutetea maslahi ya wanwake na watoto katika shehia hiyo.
Mapema mjumbe wa kamati ya kupambana na udhalilishaji wilaya ya Chake
chake Burhani Khamis Juma, alisema kuwa udhalilishaji unajumuishwa siyo tu
vitendo vinavyopelekea madhara ya kimwi, bali hata mateso na kudharauliwa.
Alisema kuwa matokeo ya udhalilishaji ni makubwa yanayoweza kusababisha majaraha, kifo, kisaikolojia, tabia hataraishi na matokeo mabaya ya kielimu na kikazi.
"Mnawajibu mkubwa wa kuzuia, kupinga na kupambana udhalilishaji, na kuna
kila aina ya kuwasaidia watoto na kueleza athari za vitendo hivyo, ili kusaidia
jamii na serikali kiujumla,"alifafanua.

Kaimu sheha wa Mvumoni Fatma Ali Khamis alisema kuwa, kuundwa kwa kamati
hiyo itahakikisha inaweka mikakati ya mizuri ya kuwasaidia wananchi wake, ili
kuonesha mfano kwa shehia nyingine juu vitendo hivyo.
Msaidizi wa sheria shehia ya Mvumoni Haji Nassor Mohamed, alisema kuwa lengo la
kuwepo kamati hizo ni kupinga na kupambana na udhalilishaji, ili kuwaweka
salama wanawake na watoto.
"Tumeunda kamati ya kupinga na kupambana na vitendo vya udhalilishaji, ili
kwenda kuisaidia jamiii kwa kuwapa elimu hiyo, na kuhakikisha wanawake na
watoto wanabaki kuwa salama, wasifanyiwe udhalilishaji,"alifafanua.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya
Chake chake Fatma Hilali Salu, alisema kuwa, Jumuiya hiyo ipo kisheria chini ya
ofisi ya Katiba na sheria, kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria bila ya malipo
kwa wananchi.
Alisema kuwa Jumuiya ipo kwa kuwasaidia wananchi wa tabaka la chini wasiyo na
kipato ili kupata haki zao kwa wakati.
Nae Mratibu wa
kamati hiyo Hawa Kassim Omar, alisema anafarajika kuzinduliwa kwa kamati hiyo,
kwani alikuwa akifanyakazi katika mazingira magumu.
Kamati hiyo imeundwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo sheha, Naibu sheha, diwani, mratibu wa shehia, msaidizi wa sheria, waalimu wa wakuu, washauri nasaha na kundi la watu wenye ulemavu.
MWISHO.







Comments
Post a Comment