WAZO LA MSAIDIZI WA SHERIA LAKUBALIWA MVUMONI
NA AISHA MOHAMED, PEMBA@@@@ MSAIDIZI wa sheria shehia ya Mvumoni wilaya ya Chake Chake Pembaa, Haji Nassor Mohamed, ameutaka uongozi wa shehia hiyo, kuifufua kamati ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, ili vitendo hivyo visiendelee kuwathiri wanawake na watoto. Msaidizi huyo wa sheria, aliyasema hayo jana kituo cha afya Mvumoni, kwenye mkutano maalum unaolenga, kuifufua kamati hiyo, na kuhudhuriwa na wajumbe wa sheha na mratibu wa wanawake na watoto wa shehia hiyo. Alisema lengo la kikao hicho ni kuja kuifufua kamati ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, ambayo ilionekana kusizi, ili kuweza kuvipunguza vitendo hivyo shehiani humo. Alisema vitendo vya udhalilishaji vipo katika shehia za wilaya ya Chake chake ikiwemo ya Mvumoni, hivyo ni wakati sasa kuifufua na wajumbe wake wake, kufanyakazi wa bidi. “Nawaomba sana wajumbe wa kamati na sheha mwenyewe, tushirikiane na mratibu wetu wa wanawake na watoto wa shehia, ili ku...