WAZO LA MSAIDIZI WA SHERIA LAKUBALIWA MVUMONI

 


NA AISHA MOHAMED, PEMBA@@@@

MSAIDIZI wa sheria shehia ya Mvumoni wilaya ya Chake Chake Pembaa, Haji Nassor Mohamed, ameutaka uongozi wa shehia hiyo, kuifufua kamati ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, ili vitendo hivyo visiendelee kuwathiri wanawake na watoto.

 

Msaidizi huyo wa sheria, aliyasema hayo jana kituo cha afya Mvumoni, kwenye mkutano maalum unaolenga, kuifufua kamati hiyo, na kuhudhuriwa na wajumbe wa sheha na mratibu wa wanawake na watoto wa shehia hiyo.

 

Alisema  lengo la kikao hicho ni kuja kuifufua kamati ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, ambayo ilionekana kusizi, ili kuweza kuvipunguza vitendo hivyo shehiani humo.

 

Alisema vitendo vya udhalilishaji vipo katika shehia za wilaya ya Chake chake ikiwemo ya Mvumoni, hivyo ni wakati sasa kuifufua na wajumbe wake wake, kufanyakazi wa bidi.

 


“Nawaomba sana wajumbe wa kamati na sheha mwenyewe, tushirikiane na mratibu wetu wa wanawake na watoto wa shehia, ili kuona sasa kamati hii, inafanyakazi zake,’’alifafanua.

 

Kwa upande wa Katibu wa Kamati ya kupambana na udhalilishaji wilaya ya Chakechake Rashid Said Nassor aliahidi kushirikiana na kamati hiyo, ili kuhakikisha vitendo hivyo haiendelei kawatesa wanawake na watoto.

 


Aidha aliahidi kuwapa elimu, mara tua atakapoarifiwa juu ya kuundwa na kuanza kazi kwa kamati hiyo ya shehia ya Mvumoni wilaya ya Chakechake.

 

‘’Katika kuinga mkono kamati hiyo, naahidi kusaidia vitendea kazi, ikiwemo karatasi na vifaa vingine, ili kamati ifanye kazi kwa ufanisi,’’alifafanua.

 

Hata hivyo aliwataka wananchi wa shehia hiyo, kumtumia kwa karibu Msaidizi wa sheria walie nae, ili kutatuliwa changamoto zao kadhaa za kisheria.

 

Akizungumzia muu wa kamati hiyo, alisema sheha wa anakuwa ndie Mwenyekiti, Mratibu wa wanawake na watoto Katibu na wajumbe wingine kutoka kila makundi yaliomo ndani ya shehia.

 


‘’Msaidizi wa sheria anakuwa mjumbe, Askari wa shehia, watu maarufu, viongozi wa dini, waalimu wakuu, mabaraza ya vijana na makundi ya watu wenye ulemavu,’’alifafanua.

 


Mapema Mratibu wa wanawake na watoto wa shehia ya Mvumoni Raisa Salim Mohamed, alisema kuwa kamati ipo ingawa, haina wajumbe, waliomo mwenye muunndo wa kisheria.


‘’Kazi nafanya kila siku, ingawa nashirikiana na wajumbe wa kamati ya sheha na wakati mwingine waalimu wa skuli na madrassa, inapohitajika,’’alifafanua.

 

Hata hivyo, alisema ipo haja ya kuwepo kwa wajumbe waliotajwa kwenye muongozo, kwani bado matendo hayo yanaripotiwa kila siku.

 


Nae Katibu wa sheha wa Mvumoni, Khamis Mohamed Abdallah, ametoa shukran kwa msaidizi wa sheria na katibu wa kamati ya kupambana na udhalilisha ya wilaya ya Chakechake, kwa kuja na wazo hilo.

 

“Kwakweli tunashukuru sana msaidizi wa sheria na katibu, maana hili jambo lilikuwa linatuumiza kichwa, hatujui nini tufanye, ingwa sasa ujio wenu tumeshapata mwanga,’’alifafanua.

 

Takwimu zilizokusanywa na Ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar, iliripoti matukio 1,809 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, kwa mwaka 2024, ambapo waathirika walikuwa 1,809 na wengi walikuwa watoto sawa na asilimia 84.3.

 


Wilaya ya Chake chake, ilishika nafasi ya nne, kwa kuripoti matukio 113, kati ya wilaya 11 za Unguja na Pemba, huku wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, ikiwa ya mwanzo kwa matukio 431.

 

Kwa mwaka jana, matukio hayo kwa Unguja na Pemba, yalipungua 581, maana yalikua 1,228, kinyume na yake 1,809 ya mwaka 2024, jambo hata baadhi ya wilaya, ikiwemo ya Chake chake, nako yaliripotiwa kushuka.

 



 

Wilaya iliyoongoza kwa mwaka jana ni Magharibi ‘A’ kwa matukio 247, na wilaya ya Chake chake safari hii, ilipanda nafasi moja, ingawa iliripoti matukio kiduchu 93, tofauti na matukio 113 ya mwaka 2024.

 

Waathirika wakubwa kwa mwaka 2025, ni watoto, waliokuwa 1,050 sawa na asilimia 85.4 kwa Unguja na Pemba, wakifuatiwa na wanawake 162 asilimia 13.2 na wanaume 18, sawa na asilimia 1.5.  

                         Mwisho

 

Comments

Popular posts from this blog

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR YAKUSANYA MAONI SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

MKURUGENZI HANIFA, AWAUMA SIKIO WANANCHI WAWI HAKI ZA BINAADAMU

‘WANANCHI HAWANA MAMLAKA YA KUONDOSHA UHAI WA MTU’